Ads (728x90)


SAMSON Simkoko Diwani kata ya Halungu aliyeibua tuhuma za Mkuu wa wilaya ya Mbozi
DC MBOZI DKT Kadeghe anayetuhumiwa kuwalambisha mshiko wanahabari

 Septemba 5 Mwishoni wa wiki iliyopita kulikuwa na taarifa za baadhi ya waandishi wa habari kulambishwa mshiko (Rushwa) kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dkt. Michael Kadeghe kwa kile kilichoelezwa kuzuia kutolewa kwa stori inayomhusu juu yua ubadhirifu wa fedha za Halmashauri ya wilaya ya Mbozi.
Tuhuma hizo kwa waandishi wa habari ziliibuka baada ya baadhi ya waandishi wa habari kutuma stori hiyo News Room ambako walitakiwa kubalance kwa Mkuu huyo ili kumpa nafasi ya kujieleza kutokana na tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.
Kwa mujibu wa maelezo ya tukio hilo ni kuwa baada ya kumalizika kwa kikao ambacho madiwani wa Halmashauri hiyo walimshambulia wazi wazi Mkuu huyo wa wilaya kwa kile kilichoelezwa kuwa ni miongoni mwa waliosababisha kupatikana kwa hati ya Mashaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Ilikuwa ni katika kikao cha kupitia Hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2013-2014 ambapo takribani hoja 100 zilikuwa bado hazijafungwa na hivyo kuonesha namna ambavyo Halmashauri hiyo imeshindwa kuwajibika vyema katika ukusanyaji wa mapato.
Ilielezwa kuwa mara baada ya kumalizika kwa kikao mmoja waandishi wa Habari(jina tunalo) alikutana na Mkuu huyo wa Wilaya ambapo ilielezwa kuwa alitengeneza ushawishi wa kukubaliana na Mkuu huyo wa Wilaya ili kumsaidia kupunguza makali ya taarifa itakayotolewa kwenye vyombo vya habari.
‘’Yule mwandishi tulimuona yuko pembeni wanateta na Mkuu wa wilaya wakizungumza kilugha ( Lugha ya asili) wakazungumza kwa muda mrefu walionesha kukubaliana jambo’’ alisema mmoja wa watoaji wa taarifa hizi aliyekuwa akifuatilia kikao hicho.
Inadaiwa kuwa mara baada ya makubaliano mwandishi alimweleza DC kuwa yeye anao uwezo wa kuwashawishi waandishi wenzie kutotoa stori hiyo hivyo ampe mshiko ambao atawagawia wenzie, DC inadaiwa akakata mshiko wa kutosha ambao hadi sasa haujulikani ni kiasi gani.
Wakati wanahabari wakiwa wanarejea Mbeya kutokea Mbozi, walikuwa katika majadiliano juu ya stori hiyo huku wakielezea namna ambavyo DC huyo alivyoshambuliwa na Madiwani na kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa maadili ya Uongozi.
Katika mjadala huo inaelezwa kuwa mwandishi anayedaiwa kulamba mshiko alikuwa amenyamaza kimya huku akichombeza maneno machache ya kuwashawishi waandishi wajaribu kumuonea huruma mkuu huyo kwa kutoandika habari kali.
Hata hivyo inaelezwa kuwa alipoonm msimamo wa waandishi hao juu ya kuandika stori hiyo, kesho ya Septemba 6 asubuhi aliwapigia baadhi ya waandishi na kuwaeleza kuwa amepewa hela na Mkuu wa wilaya ili isiandikwe stori hiyo.
Baadhi ya waandishi(majina tunayo) walikiri kupigiwa simu na mwandishi huyo na kudai kuwa alipewa fedha kiasi cha shilimgi Laki moja( 100,000) ili awagawie waandishi wa habari kila mmoja elfu ishirini(20,000) kati ya waandishi watano na kuwa waandishi wengine watano waliobaki stori zao hazina impact kubwa hata kama wataandika.
Mmoja wa waandishi ambaye aliandika stori yake na kuituma News Room kwake alipigiwa simu na Mhariri wake kwamba anapaswa kuibalance stori hiyo kwa Mkuu wa wilaya ambaye ametuhumiwa na Madiwani, alipompigia DC huyo ili kuibalance alidai kuwa Mkuu huyo alimuuliza kama hajawasilana na wenzie.
‘’Nilipompigia ili kuibalance alishangaa na kuniuliza  vipi Bwana Mdogo hujawasiliana na ……. ?(alitaja jina la mwandishi aliyepewa mshiko ili awagawie wenzie).
‘’Mie nilishituka sana kuambiwa huyu..(alitaja jina la Mwandishi) kuwa amelamba mshiko halafu amekaa kimya bila kuwaeleza wenzie,lakini hata hivyo DC ni mtu mmoja na Madiwani ni wengi wanawawakilisha wananchi wapatao laki nne, kumbeba DC na kuwatosa wananchi wengi sio fare kabisa,’’alisema Mwandishi huyo.
Septemba 7 ikiwa imepita  siku mbili baada tukio hilo mwandishi wa Blogu hii alipigiwa simu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Elick Ambakisye na kuelezea masikitiko yake juu ya kitendo kilichofanywa na waandishi wa habari kula rushwa.
Ambakisye alielekeza lawama zake moja kwa moja kwa waandishi huku akitaja jina la Mwandishi aliyedaiwa kushikishwa MSHIKO na DC na kusema kuwa kikao kizima cha Halmashauri ya Chama kiliwatupia lawama waandishi na kudai kuwa upo ukweli wa jambo hilo kwa kuwa hakuna chombo hata kimoja kilichotoa stori ya kikao hicho.
Aidha Ambakisye alisema kuwa hata hivyo kikao hicho hakikumalizika salama kutokana na taharuki iliyokuwepo kati ya Madiwani na DC na kuahirishwa hadi siku ya pili.
Septemba 8  Mwanablogu wetu alitinga wilayani humo na kukuta kikao kikiendelea ambacho kilikuwa na mvutano mkubwa kati ya Uongozi wa CCM wilaya na Madiwani wa Halmashauri hiyo wakiwemo watendaji wa Halmashauri ya wilaya, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa chama wilaya.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM mkoa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi ambapo hatima ya kikao hicho ambacho kiliwashutumu Madiwani kutowajibika vyema katika kuwasimamia watendaji wa Halmashauri hiyo, ilipendekezwa wajiuzuru nafasi zao.
Wakiwa nje mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa George Mwenisongole alitoka nje ya kuwaeleza wanahabari kuwa baadaa ya kikao hicho atakuwa na maneno ya kuzungumza na waandishi ambapo pia alitoa tahadhari kwa kusema kuwa lakini wasifanye kama alivyofanya mwandishi( alimtaja jina) aliyechukua mshiko kwa DC.
‘’Nitaongea nanyi baada ya kikao ila msifanye kama mwenzenu(alimtaja jina) amechukua habari then akaenda kulamba mshiko kwa DC hiyo sio fare ndugu zangu tunawategemea kama kioo cha jamii na kisemeo cha wanyonge,’’alisema Mwenisongole.
Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho nje ya ukumbi Mkuu wa Wilaya alipotoka na kuonana uso kwa uso na Waandishi wa Habari alionesha dhahiri kuwalaumu kutokana na Stori iliyosoma kwenye moja ya Televisheni mchana wa siku hiyo
‘’ Mmenidhalilisha sana pamoja na kujipendekeza kwangu kwenu, lakini mmetoa ile habari mme ni –demoralized sana okay mmeamua kuitoa hiyo stori yaani pamoja na kujiwekea urafiki na ninyi mmeamua kunifanyia hivyo? alilalamika Dkt.Kadeghe mbele ya waandishi wachache waliokuwepo nje ya ukumbi wa CCM wilayani humo.
Hata hivyo taarifa za kupewa mshiko kwa waandishi na DC kumeelezwa ni tamaa ya waandishi hao iliyotokana na ukata na kuwa inaelezwa kuwa Mwandishi aliyekula mshiko alifanya hivyo kwa nia ya kujiongezea kipato kwa njia zisizo halali na hivyo kuweka pembeni taaluma yake kwa kujinufaisha.
Mwanablogu wetu hakuishia hapo alim -face moja kwa moja mwandishi aliyetuhumiwa kulamba MSHIKO kutoka kwa DC kwa nia ya kuzima soo yake, Mwandishi huyo pamoja na kutajwa wazi wazi kuhusika na sakata hilo alikanusha macho makavu na kudai kuwa yeye hawezi kufanya jambo hilo.
MWANABLOGU: Lakini unadaiwa kuhusika moja kwa moja na skendo hii na umetajwa jina lako,unasemaje kuhusu suala hilo.
MWANDISHI: Hayo  ni majungu tu, mie sijahusika kabisa, tena kule kuna stori nyingi sana ukiacha hiyo skendo mie nikiamua nitaandika mabaya zaidi ya hayo.
MWANABLOGU: Lakini unaelezwa kuwa ulikuwa umekaa pembeni unazungumza kilugha na DC umesikika na watu wamekuona, hilo unalizungumziaje.
MWANDISHI: Pale niliposimama tulikuwa mimi, DC na Mkuu wa Mkoa Mzee Kandoro, hatukuwa na nafasi ya kuteta kwa lugha yoyote pale nilikuwa Napata ufafanuzi juu ya kikao kile lakini si hayo unayoniuliza.
MWANABLOGU: Inadaiwa kuwa mmelamba mshiko na Stori hamjaandika,unaweza kunieleza kwanini hamkuandika stori kubwa na yenye hisia za kijamii kama ile, kutoandika kwa stori hauoni kuwa itahalalisha kuwa mmelamba mshiko?
MWANDISHI: Mie nilichelewa kutuma stori yangu, wala si kwa ajili ya kulamba mshiko, potelea mbali kama nitaeleweka vinginevyo, stori hazipo Mbozi pekee yake ninaweza kwenda kufanya katika wilaya nyingine, tena wana skendo nyingi sana wale nikiamua kuandika wataumia sana.

Post a Comment