Ads (728x90)


Kuna wakati pamoja na kutumia magari yetu matatu, BENZ, NOAH na GAIA tulilazimika kupumzika na kupunga upepo hatukuwa na haraka katika safari yetu ya kihistoria iliyounganisha mahusiano ya nchi mbili zilizokuwa zikipigana vita vya maneno kupitia baadhi ya vyombo vya habari.

Tulibadilishana mawazo tukiwa ugenini nchini  Malawi kuna wakati tulianza kukumbuka nyumbani

Tulitumia fursa hiyo kuwasiliana na wenzetu wa nyumbani Tanzania na kuwajulisha kila kinachoendelea katika safari yetu, tulifanya hivyo tukiwa ndani ya magari yetu na hata tuliposimama kwa ajili ya mapumziko mafupi, kwa ujumla safari yetu ilikuwa wazi wadau na ndugu zetu wa nyumbani walituona online kila hatua tulioyoipitia.

Tulijisikia njaa tulikula chakula chetu tulichojiandalia kwa safari nzima, Kuku wa kukaanga, ndizi choma na vinywaji ambavyo wadau wenzetu wa habari uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari mko wa Mbeya(Mbeya Press Club) walituchangia

Hatukula chakula peke yetu bali watoto tuliokutana nao njiani nao walifaidika na chakula tulichoandaa, walifurahia mlo huo na kutushukuru kwa lugha ya kwao ZIPOMA KWA MBILI
Kwa kweli ilikuwa ni baraka kuu ya safari yetu kutoka kwa watoto hao, mratibu wa safari Venance Matinya alikuwa akiwagawia watoto hao chakula, i njia nzima tulisafiri kwa raha mustarehe
Tulipongezana kwa kukanyaga ardhi ya Malawi pembezoni mwa Ziwa Nyasa, hapa Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu na Freddy Njeje moderetor wa Mbeya Yetu na Tone Multimedia na Blog za Mikoa wakifurahia kuikanyaga ardhi ya Malawi.
Ilikuwa ni furaha ya aina yake kuwepo ugenini bila kikwazo chochote njiani
Hata hivyo tulichukua tahadhari kwa kuondoa mikosi, husuda za wale ambao hawakututakia mema katika safari yetu, tulinawa mikono na kuucha mikosi yote ndani ya Ziwa Nyasa, safari ilikuwa murua na salama.
Hakuna mmoja kati yetu aliyepata matatizo yoyote katika safari yetu, hakuna aliyeugua kichwa wala mafua sote tulikuwa salama katika safari yetu ndefu.
Wenyeji wa Malawi ambao kiasili walionesha ukarimu wa hali ya juu walituelekeza maeneo, baadhi yao hawakujua lugha ya Kiingereza wala kiswahili tulilazimika kuongea nao kwa ishara na kwa kuwa baadhi ya lugha zetu za kibantu zinafanana tulijikuta tukielewana kwa lugha zetu za asili.
Tuliliacha Ziwa Nyasa na kuendelea na safari yetu!!!!

Post a Comment

Post a Comment