Ads (728x90)

Mbunge wa MBEYA mjini Joseph Mbilinyi, Sugu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia ya chama hicho kumtaka RPC Ahmed Msangi ajiuzulu wadhifa wake kwa kile alichodai kuwa ana nia mbaya na wafuasi wa CHADEMA.
Sugu alisema kuwa Kamada Msangi amenukuliwa na gazeti moja la kila siku kuwa iwapo wafuasi wa CHADEMA wangeandamana angewafanyia kitu mbaya.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya mjini John Mwambigija alidai kuwa RPC Msangi anatumika kisiasa na kuwa kitendo chake cha kusema kuwa anawafanyia kitu mbaya wanachadema kitasababisha uvunjifu wa amani na kuwa ili kuepuka suala hilo anapaswa kukanusha kauli yake.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA Moses Mwaifunga alisema kuwa Vijana wamejiandaa kwa lolote ambalo polisi watakalodhamiria na kuwa vwanaamini Jeshi la Polisi haliwezi kutumika kwa maslahi ya wanasiasa.

''Ninajitambua siwezi kufanya jambo kama hili, mimi ni ofisa wa Polisi kwa muda wa miaka 20sijatamka kitu cha namna hiyo mwenyewe niliona kwenye gazeti, niwape pole CHADEMA kwa usumbufu walioupata kutokana na jambo hili nadhani limeongezwa chumvi, ninafanyakazi na hawa jamaa kwa karibu, ninawatambua ninawafahamu, tunawaheshimu nimeshirikiana nao sana,''alisema RPC Msangi.
 
 

Post a Comment

Post a Comment