Kikosi cha timu ya Azam FC kilichowalambisha Mbeya City bao 1-0 katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya leo jioni |
Kikosi cha Mbeya City kilichokubali uteja wa kufungwa mara mbili mfululizo na timu ya Azam ya Jijini Dar |
Kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Mbeya City na Azam |
MABINGWA
watetezi wa kombe la Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita Azam FC leo imeendeleza
ubabe kwa kuifunga timu ya Mbeya City ya Jijini Mbeya kwa bao 1-0.
Msimu
uliopita Azam iliweza kuifunga Mbeya City mabao 2-1 katika uwanja wake waw
nyumbani na kuipa tiketi ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu timu
hiyo ianzishwe.
Katika mechi
ya leo timu hizo zilianza kwa kushambuliana kwa zamu huku kila mmoja akionesha
uchu wa kuishinda mechi hiyo.
Azam
iliyoongozwa na washambuliaji Kipre Cheche,Erasto Nyoni,Didier Kavumbagu, Himid
Mao na Micheal Ballou iliutawala mchezo katika kipindi cha mwanzo huku Mbeya
City ikiwategemea walinzi wake Deogratius Julius,Hassan Mwasapili, Yusuf
Abdallah na Yohana Morris kuzuia mashambulizi ya wachezaji wa Azam.
Ilikuwa ni
katika dakika ya 19 ya mchezo kulipotokea mashambulizi langoni kwa Mbeya City
ambapo mchezaji wa Azam Salum Abubakar ‘Sure Boy’ alifanyiwa madhambi eneo la
adhabu na mwamuzi Martin Sanya aliamuru upigwe mpira wa adhabu ndogo kuelekea
kwa timu ya Mbeya City.
Mpira huo
uliopigwa na Aggrey Morris ulitinga moja kwa moja wavuni kupitia juu na
kumuacha golikipa wa Mbeya City David Burhan akichupa bila mafanikio.
Goli hilo la
Azama lilizima nderemo na hoi hoi za mashabiki wa Mbeya City na kuibua vifijo
na nderemo kwa upande wa mashabiki wachache wa Azam walioketi katika jukwaa la
kusini.
Baada ya
goli hilo wachezaji wa Mbeya City alionekana kutoelewana na kulazimika kucheza
mipira ya juu juu na mara nyingine kupiga ovyo bila mpangilio huku wachezaji wa
timu ya Azam wakicheza kwa kuonana.
Ilikuwa
almanusura kwa timu ya Azam ihesabu bao la pili katika dakika ya 26 ya mchezo ambapo
hata hivyo mwamuzi alinyoosha kibendera cha kuotea kabla ya mchezaji wa Azam
Said Morad hajatumbukiza mpira wavuni.
Hadi
mapumziko Mbeya City ilikuwa nyuma kwa 0-1 ya bao la Azam.Kipindi cha pili
kilianza kwa kasi huku Azam wakitaka kuongeza bao na Mbeya City wakijitahidi
kutafuta bao la kusawazisha lakini bahati kwa Mbeya City haikuwa yao.
Kipenga cha
mwisho cha mchezo kilishuhudia mashabiki wa Mbeya City wakitoka vichwa chini na
kukubali kuwa vibonde wa Azam kwa mara ya pili mfululizo kwa kufungwa bao 1-0.
Mbeya City:
David Burhan,Deogratius Julius,Hassan Mwasapili,Yusuph Abdallah,Yohana
Morris,Antony Matogolo,Saad Kipanga,Steven Mazanda,Paul Nonga, Mwagane Yeya na
Deus Kaseke.
Azam FC: Aishi Manula,Shomar Kapombe,Gadiel
Mbaga,Said Morad,Aggrey Morris,Michael Ballou,Himid Mao,Erasto Nyoni,Didier
Kavumbagu,Salum Abubakar na Kipre Cheche.
Post a Comment
Post a Comment