Ads (728x90)

Kikosi cha Tanzania Prison kilichohceza na Simba leo jioni.
Kikosi cha Simba kilichochuana vikali na timu ya Tanzania Prison uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine leo jioni
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lililofungwa na Emmanuel Okwi
Makocha Patrick Phiri wa Simba na David Mwamwaja wa Simba kabla ya kuanza kwa mechi hiyo
Timu ya Simba ya Jijini Dar es salaam imeshindwa kutamba mbele ya maafande wa Magereza Tanzania Prson baada ya kulazimishwa sare ya 1-1.
Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kujipatia bao katika dakika ya pili ya mchezo baada ya Emmanuel Okwi kutikisa wavu kwa njia ya adhabu ndogo.Adhabu hiyo ilitokana na mchezaji wa Prison Lugano Mwangama kumfanyia madhambi mlinzi wa Simba Ramadhani Singano.
Hadi mapumziko Simba ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya pande zote huku wachezaji wa Simba wakicheza kwa kupoteza muda hasa golikipa wa timu hiyo Peter Manyika.
Poteza muda ya wachezaji wa Simba iliwaponza katika dakika ya 89 ya mchezo ambapo golikipa Peter Manyika na walinzi wa timu hiyo walijisahau kuwa mchezo unaendelea na kuruhusu goli lililofungwa na Hamisi Maingo ambaye aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Jeremia Juma.
Kwa kipindi chote washamngiliaji wa timu ya Simba ambao waligawanyika katika makundi mawili walionekana wakiishangilia timu yao bila kuchoka hadi pale timu yao iliporuhusu bao la kusawazisha la Prison.
Hadi kipyenga cha mwisho cha mwamuzi Athuman Lazi kutoka mji kasoro Bahari (Moro) kinapulizwa Simba 1Prison 1.

Post a Comment

Post a Comment