Muonekano wa juu wa mabanda ya biashara katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya siku ya mwisho ya maonesho hayo Ockoba 29 |
Bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zilizagaa Jijini Mbeya ambapo wakazi wa Jiji la Mbeya walifanikiwa kununua bidhaa hizo kwa bei rafiki |
Wajasiriamali mbalimbali walijitokeza kuuza bidhaa zao katika ukumbi wa Mkapa ambao kwa takribani wiki nzima uligeuka kuwa duka la aina yake la bidhaa mbalimbali za ndani na nje ya nchi |
Wajasiriamali kutoka nchi za kigeni hawakuwa nyuma kuonesha namna ambavyo nyenzo rahisi za kurahisisha ukataji wa viungo vya vyakula vilivyoweza kufanya kazi |
Ilikuwa ni fursa pekee ya kujipatia bidhaa hizo ambazo ni nadra kupatikana katika mazingira tuliyoyazoea |
Bidhaa mbali mbali za urembo kwa akina mama zilizagaa katika maonesho hayo na kuwa nafasi pekee kwa akina mama wa Jiji la Mbeya kujipatia bidhaa hizo |
Wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya hawakuwa nyuma kuonesha na kuuza bidhaa zao kama inavyoonekana pichani |
Muda wote wa maonesho hayo viongozi wa TCCIA walikuwa wakifuatilia na kuratibu maonesho ili kuweka kumbukumbu sahihi za uoneshaji na kupata uzoefu kwa ajili ya maonesho ya aina hiyo wakati mwingine. |
Mjasiriamali kutoka Jijini Dar es salaam akikaribisha wateja katika banda lake la maonesho kwenye viwanja vya maonesho ya biashara yaliyohitimishwa Oktoba 29 Jijini Mbeya |
Post a Comment