Mashabiki wa Mbeya City wakiingia kwa mbwembwe |
LIGI kuu ya
Vodacom imeendelea katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya kwa kuwakutanisha
mahasimu wawili wenyeji wa Mbeya timu ya
Jeshi la Magereza Prison na Mbeya City na kutoka sare ya bao 2-2.
Prison
iliyokuwa katika hali mbaya kwenye msimamo wa ligi ambayo kabla ya mchezo huo
ilikuwa na jumla ya pointi 9 huku wenzao Mbeya City wakiwa na pointi 11 ndiyo
ilikuwa ya kwanza kuliona lango la Mbeya City katioka dakika ya 5.
Goli hilo la
Prison lililofungwa na Boniface Hau liliwachanganya wachezaji wa Mbeya City na
kucheza bila kuelewana katika dakika hizo za mwanzo za mchezo.
Hau aliyevalia
jezi nambari 3 mgongoni aliambaa ambaa na mpira upande wa kulia na kuwatoka
walinzi wa Mbeya City Paul Nonga na Boniface Fred na hatimaye kupiga shuti
lililomwacha golikipa wa Mbeya City David Burhan akichupa bilaa mafanikio.
Goli hilo la
Prison liliamsha hisia mpya kwa mashabiki wa Prison huku wenzao wa Mbeya City
ambao waliingia uwanjani kwa mbwembwe wakibaki kimya wakiwa wamelowa mithili ya
waliomwagiwa na maji.
Kwa kipindi
chote cha mchezo dakika za mwanzo Prison walionekana wakisakata kambumbu safi wakitoa
mashambulizi kwa zamu ilhali wachezaji wa Mbeya City wakijaribu kuchomoa
mashuti yaliyokuwa yakielekezwa golini kwao.
Mbeya City
walikuwa wakipeleka mashambulizi machache katika lango la Prison lakini ambapo
katika dakika ya 42 Paul Nonga wa Mbeya City aliipatia timu yake bao la
kusawazisha baada ya wachezaji wa Prison kuzubaa na kutitumia fursa hiyo
kufunga bao ambalo golikipa wa Prison Mohamed Yusuf aliudaka kisha akautema.
Bao hilo
liliamsha nderemo na vifijo kwa mashabiki wa Mbeya City huku wenzao wa Prison
wakitaharuki wasiamini kuingia kwa bao hilo.
Hadi
mapumziko timu zote zilitoka uwanjani kwa kufungana bao 1-1.
Kipindi cha
pili cha mchezo kilianza kwa kasi hukun wachezaji wa Mbeya City wakionyesha
uchu wa kupata bao la kuongeza ambapo katika dakika ya 48 ya mchezo mchezaji
aliyevalia jezi nambari 7 mgongoni Themi Felix aliwainua tena mashabiki wa
Mbeya City kwa kufunga bao baada ya wachezaji wa Prison kujisahau kwenye safu
ya ulinzi.
Felix
alifunga bao hilo huku akisindikizwa na walinzi wa Prison ambapo alipiga shuti
la mbali lililotinga wavuni upande wa kushoto ambapo golikipa Mohamed Yusuf
alichupa bila mafanikio.
Baada ya
kuingia kwa goli hilo wachezaji wa Mbeya City walionekana wakiwa wamepata ari
mpya ingawa dakika kadhaa zilikuwa zikipotezwa bure na golikipa wa Mbeya City David
Burhani aliyekuwa akiudaka mpira na kulala chini muda mrefu.
Kunako
dakika ya 55 ya mchezo Meshack Seleman nusura alipatia timu yake bao la
kusawazisha baada ya kubaki yeye na golikipa David Burhani lakini alipiga mpira
uliotoka juu ya goli.
Wakati Mbeya
City wakiwa na matumaini ya ushindi wa mchezo huo kutokana na kupoteza muda,
wenzao wa Prison waliongeza spidi ili kujipatia bao la kusawazisha ambapo
zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kumalizika mchezaji wa Prison Nurdin Chona
aliipatia bao safi timu yake.
Goli hilo
liliingia baada ya kumhadaa golikipa na walinzi wa Mbeya City na kuupiga mpira
uliopenya katikati ya mikono na kichwa cha golikipa na kutinga wavuni.
Hata hivyo kabla
ya kupuliza kipyenga cha kuumaliza mpira mwamuzi wa mchezo huo Simon
Mbelwa(PWANI) alimzawadia kadi nyekundu mchezaji wa Prison Hamis Maingo baada ya
kupigana na mchezaji wa timu ya Mbeya City Juma Nyoso hali ambayo ilizusha
tafrani miongoni mwa wachezaji wa Prison wakidai kuwa kadi hiyo imetolewa kwa
uonevu.
Hadi mpira
unaishi timu zote zimetoka nguvu sawa kwa bao 2-2
Post a Comment
Post a Comment