Ads (728x90)

Nimejifikiria sana!!! hivi haya ni maisha stahiki kwa familia zetu, watoto hawa wako kwenye dampo la takataka  wakiokota masazo yaliyosazwa na watu wengine,


Kama wazazi wao wapo kwanini wako huku majalalani wakati huu muda wa masomo badala ya kwenda shuleni

Inawezekana kweli hawana wazazi, jee wanatokea wapo wanapokuwa huku, walezi wao jee, au ni michezo ya kitoto? Jamii inayowazunguka wanayaona haya, wamechukua hatua gani?

Natafakari inawezekana kuwa ni michezo ya kitoto? wanatoroka shule na wazazi wao hawajui, au wazazi wao wakiwa kazini wao hutorokea mitaani, sijapata jibu hadi sasa, natafakari maisha haya!!!!

Post a Comment

Post a Comment