Mashabiki wa Yanga wakishangia ushindi wa timu yao. |
Yanga ya Dar es salaam jana imetoa kichapo kikali dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza Prison na kujikusanyia jumla ya Point 28 na kukali kiti cha ligi hiyo kwa kuifunga timu hiyo jumla ya mabao 3-0.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ulianza kwa kasi ambapo Yanga ndio waliotawala zaidi mchezo kuliko wenyeji wao Prison.
Ililkuwa ni dakika ya 3 ya mchezo Mchezaji wa Yanga Saimon Msuva aliwainua wapenzi wa timu hiyo vitini kwa kushangilia bao la kwanza ambalo lilipatikana baada ya kona maridadi iliyopigwa na Mbrazil Andrew Cotinho.
Bao hilo liliamsha hisia kwa wachezaji wa Yanga ambao walianza kulishambulia lango hilo kama nyuki huku wachezaji wa Prison wakiwa wamepotezana ambapo walishindwa kulifikia goli la Yanga na kuishia njiani baada ya mabeki wa YangaOscar Joshua,Juma Abdul,Nadir Canavaro na Kevin Yondani kuweka ulinzi wa kutosha langoni.
Ni mara chache wachezaji wa timu ya Prison walifanikiwa kulifikia lango la Yanga ambapo michomo hafifu iliyopigwa na wachezaji wa Prison akina Jacob Mwakalobo,Boniface Hau na Fred Chudu ilipanguliwa na mingine kudakwa na golikipa wa Yanga Ali Mustapha(Baltez).
Ilikuwa ni dakika ya 12 ya mchezo huo ambapo Mbrazil Cotihno alidhihirisha umahiri wake kwa kufunga bao safi baada ya kupokea krosi ya Amis Tambwe ambayo ilimkuta Msuva na atimaye kumfikia kisha akapiga shuti iliyomchanganya golikipa wa Prison Mohamed Yusuf na mpira kutinga wavuni.
Goli hilo la pili kwa Yanga lilizidi kuwachanganya wachezaji wa Prison huku wakicheza bila kuelewana huku mashabiki wakishijika vichwa kwa taharuki wasiamini kinachoendelea uwanjani.
Hadi mapumziko Yanga ilitoka uwanjani ikiwa kifua mbele kwa bao 2-0 dhidi ya wenyeji Prison.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ile ile ya kipindi cha kwanza ambapo dakika 58 ni Yanga tena ililiona lango la Prison baada ya Msuva kwa mara nyingine kupokea pasi iliyopigwa kwa kichwa na Mbrazil Cotihno na kutingisha wavu wa Prison na kuandika bao la 3-0.
Prison ambayo ilijipatia nafasi kadhaa za wazi golini mwa Yanga na kushindwa kuzitumia na baadaye ngoma kuwageukia wenyewe na hata kutaka kujifunga ambapo katika dakika 48 mchezaji Salum Kimenya nusura ajifunge bao alipokuwa akijitahidi kuokoa shuti lililopigwa na Cotihno na mpira kupaa juu ya goli la Prison.
Dakika 51 mchezaji Jacob Mwakalobo alikosa baao lawazi alipokuwa uso kwa uso na golikipa wa Yanga Baltez na kupiga mpira uliopaa juu ya mwamba.
Ilikuwa ni kama vile la Kuvunda Halina Ubani kwa Prison kwani zikiwa zimesalia dakika 3 kipyenga cha mwisho kupulizwa na mwamuzi Zacharia Jacob kutoka Pwani Jeremiah Juma wa Prison alikosa bao la wazi akiwa amebaki yeye na golikipa Baltez ambapo alipiga shuti lililodakwa kiurahisi na golikipa huyo.
Hadi Kipyenga cha kumaliza mchezo huo kinapulizwa Yanga walikuwa wakiongoza kwa bao 3-0 dhidi ya Prison.
Post a Comment
Post a Comment