WAZIRI Mkuu
Mizengo Pinda na Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe watafanya
ziara mkoani Mbeya kila mmoja kwa dhamira yake na malengo yake kwa ajili ya
kuimarisha chama chake.
Wakati
Waziri Mkuu anatarajia kuanza ziara yake kuanzia Februari 23 itakayodumu kwa
wiki moja, Mbowe ameanza ziara yake jana ambayo itadumu kwa siku nne na
kumalizia mkoani Njombe.
Akizungumzia
ziara ya Mbowe Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu alisema kuwa
ziara ya Mbowe imelenga kuwahamasisha wananchi kujitokeza katika kujiandikisha
kwa ajili ya kupiga kura Oktoba mwaka huu.
Aidha
Mwalimu alisema kuwa Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA) umeendeleea kuelezea
azma yake ya kususia zoezi la upigaji kura wa ajili ya kupitisha Katiba
iliyopendezwa kwa madai kuwa Katiba hiyo haina tija kwa Watanzania na itadumu
kwa muda wa miezi minne tu.
Mwalimu alisema
kuwa mustakabali wa KATIBA na uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu unategemea
kupigiwa kura na wananchi na kuwa wao wataendelea kususia na kuwahamisisha
wananchi kutopigia kura katiba hiyo kwa kuwa haina tija kwa wananchi.
‘’KATIBA inayotaka kupigiwa kura ni ya
serikali ya CCM sisi tumeikataa na tutaendelea kuikataa, itadumu kwa miezi
minne tu kwa kuwa Novemba Mosi Rais wa UKAWA ataingia Ikulu na kuapishwa,’’alisema
Mwalimu.
Mwalimu
ambaye pia alitoa ratiba ya ziara ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe
alisema dhamira ya UKAWA na upinzani kwa ujumla ni kuona wananchi wananufaika
na KATIBA yao hivyo si vyema kuburuzwa kutokana na mahitaji na umuhimu wa
katiba hiyo kwa miongo mingi ijayo.
Alisema kuwa
Mbowe atafanya ziara ya siku nne katika mikoa ya Mbeya na Njombe kwa ajili ya
uzinduzi na uhamasishaji wa uandikishaji wapiga kura na kuwa lengo ni kuona
wananchi wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kutumia haki zao za msingi za
upigaji kura ifikapo Oktoba mwaka huu.
Akielezea kuchelewa
kutangaza mgombea wa UKAWA kama kuna uhusiano wowote wa kusubiri mgombea
atakayeachwa na CCM kwenye kura za maoni, Mwalimu alisema kuwa katika wagombea
wanaotajwa kuwania urais ndani ya CCM hakuna hata mmoja mwenye sifa ya
kushindana na Mgombea wa UKAWA.
Alisema
taratibu za UKAWA zinaendelea huku mchakato wa kila chama ukiendelea bila
kuathiri mipango waliojiwekea na kuwa wananchi watarajie kumpata mgombea bora
kutoka UKAWA ambaye atazima kilio cha muda mrefu cha kumpata rais bora wa
Tanzania.
Wakati huo
huo taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa vyombo vya habari
imeleeza kuwa Waziri Mkuu Pinda anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika
Halmashauri 7 za mkoa huo kwa ajili ya kutembelea miradi na mikutano ya
hadhara.
Kwa mujibu wa
taarifa hiyo, Waziri Pinda atatembelea
Halmashauri ya Jiji la Mbeya,Halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Kyela,
Busokelo, Rungwe, Chunya na Mbozi ambapo atakagua miradi na kuweka mawe ya
msingi ikiwa ni pamoja na kuzindua miradi katika elimu, afya, ujenzi, barabara
na kilimo.
Post a Comment
Post a Comment