Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye,
akiingia ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es
Salaam leo asubuhi akiwa ameongozana na mke wake Ester Frederick Sumaye
kwa ajili ya kutangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wakati ukifika
iwapo jina lake litapitishwa na chama chake cha
CCM.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akiwa
na mke wake
Ester Sumaye wakati wa mkutano huo wa kutangaza nia.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (kulia), akizungumza na
wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia
hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (katikati),
akiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kiluvya,
Juma Semendu Nauchiwa. Kada wa CCM, Shabani Uronu, Mama Ester Sumaye na
Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Charles Kaenja.
Mwanahabari Ibrahim Yamola akimuuliza
swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi
hiyo.
Mwanahabari Mariam
Mziwanda akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia
ya nafasi hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau mbalimbali
wakiwa kwenye mkutano huo.
Msanii Oscar Nyerere akitoa burudani
katika mkutano huo.
Wananchi wakimpongeza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye baada ya
kuzungumza nao.
Msanii Shafii Omari akitoa burudani.
Makada wa CCM na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye ametangaza
nia ya kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa
Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar leo.
Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia akiwa Dar es
Salaam maana anataka kuwatumikia Watanzania wote siyo wa nyumbani kwake pekee.
Kauli mbiu yake ni ‘Uongozi Bora, Komesha Rushwa,
Jenga Uchumi’.
Kiongozi
huyo amesema ametangaza nia baada ya kujipima, akajitafakari na kujiridhisha
kuwa anatosha kuwania nafasi hiyo.
Sumaye amesema dira ya taifa katika miaka 10 ijayo ni
kwamba Tanzania ifikie uchumi wa kati.
Aidha kiongozi huyo ametumia muda huo kuelezea
kiongozi anayetakiwa na Watanzania kuwa:
-Kwanza ajipime, ajitafakari na ajiridhishe kuwa
anatosha nafasi hiyo
-Ajipime kiafya, kiakili, kimaadili na kidhamira
-Mzalendo, anayejua tulipotoka na tunapotaka kufika
-Kiongozi ambaye ni mtumishi atakayewatumikia wananchi
na si bosi
-Kiongozi anayefikiri na kushauriwa
-Kiongozi anayeweka maslahi ya Tanzania mbele na si
yake binafsi
-Kiongozi atakayelinda amani ya Tanzania na Muungano
wake.
-Mwenye uwezo wa kusimamia uchumi
-Atakayeboresha huduma za jamii zisizobagua watu.
-Atakayesimamia elimu ya Tanzania kurejea ilipokuwa
hapo awali na kuiendeleza zaidi
-Atakayepambana na rushwa, ujangili na madawa ya
kulevya.
Mhe. Sumaye pia amewatupia swali baadhi ya makada wa
CCM waliotangaza nia na kudai kuwa wanauchukia umasikini hivyo kuamua kuutafuta
utajiri Ikulu ambapo amewataka kama wanataka utajiri upo mitaani waende
wafungue makampuni. (Habari wa Hisani ya Global Publishers) na www.habarizajamii.com
Post a Comment
Post a Comment