MWANAMAMA
pekee mtia nia wa Ubunge Jimbo la Busokelo,Kamishna Ardhi Msaidizi Kanda ya
Pwani Suma Mwakasitu(53) amejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika
jimbo hilo kwa tiketi ya CCM ambalo awali lilikuwa chini ya Profesa Mark James
Mwandosya.
Akizungumza kwa
kujiamini na kuonesha nia ya dhati ya kupokea kijiti cha Prof. Mwandosya ambaye
aliaga rasmi jimbo hilo baada ya kuweka nia ya kuwania nafasi ya Urais wa
Jamhuri ya Muungano,Bi. Mwakasitu alisema anawiwa moyoni mwake kuwatumikia wana
Busokelo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
‘’Mimi ni
mwana Rungwe, ni mkazi wa jimbo la Busokelo nimeona ni vyema nikajitokeza
kuchukua fomu ya kuwania Ubunge ili niendeleze pale alipoishia Prof. Mwandosya,’’
alisema.
Alisema
jimbo hilo limejengwa na kuachiwa misingi mizuri na aliyekuwa Mbunge wa wake na
Waziri wa Ofisi ya Rais Kazi Maalum Prof. Mwandosya na kuwa anahitajika mtu
makini kuendeleza pale alipoachia na kuwa anaamini yeye anatosha kumpokea
kijiti na kusukuma mbele zaidi maendeleo ya jimbo hilo.
‘’Mimi siku
zote huwa naliita jimbo hili kuwa ni Small Paradise kutokana na kuwepo na uoto
wa asili wa rangi ya kijani kibichi, ardhi yetu yenye rutuba inastawi kila aina
ya mazao, anahitajika mtu makini kusimamia na kuendeleza hayo,’’alisema.
Alisema yeye
amekuwa mwanamama pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo ya Ubunge wa jimbo
tofauti na akina mama wengine ambao wamejitokeza kuwania Ubunge wa Viti maalum
na kuwa ameamini dhamira yake imesukumwa na utashi wake na hamasa ya maendeleo
ya Jimbo hilo.
Alibainisha
kuwa zipo fursa nyingi ambazo wanawake wanaziweza pamoja na woga walionao wa
kuthubutu katika fursa zilizopo.
Aidha Bi.
Mwakasitu alisema anatupa karata hiyo kuomba ridhaa ya chama chake kumsimamisha
agombee ubunge na kuwa hata kama kura hazitotosha atamuunga mkono mgombea
atakayeteuliwa na chama chake.
Kwa upande
wake Katibu wa CCM wilayani Rungwe Bi.Mariam Yusuf alisema kuwa wilaya ya
Rungwe alisema kuwa wilaya hiyo ina majimbo mawili la Rungwe na Busokelo ambapo
hadi sasa jumla ya watia nia 15 wamejitokeza kuomba nafasi za Ubunge kwa
majimbo yote mawili.
Alisema kuwa
hadi leo asubuhi jimbo la Rungwe walijitokeza wagombea saba ambao ni Kigula
Mwambene,Obadia Ndangali,Zacharia Mwansasu,Joel Mwakila, Richard Kasesela,
Mfanyabiashara maarufu nchini Sauli Amon maarufu kwa jina la S.H. AMON,na aliyewahi
kuwa mbunge wa Kigamboni kwa tiketi ya CUF kabla ya kurejea CCM Frank Magoba.
Kwa upande
wa jimbo la Busokelo Bi. Yusuf aliwataja wagombea nane waliojitokeza ambao ni
pamoja na Issa Mwakasendo,Ezekiel Mwakyambo,Juma Kaponda,Lusubilo
Mwakabibi,Steven Mwakajumilo,Ali Mwakibolwa, Aden Mwakyonde na Bi. Mwakasitu.
|
Post a Comment
Post a Comment