Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram wamezindua kiwanda wanachotumia kuunda mabomu na silaha zingine kali Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kupitia kwa mtandao wa WhatsApp picha hizo zilitumwa kwa idhaa ya Hausa ya BBC kupitia kwa namba iliyosajiliwa nchini Cameroon.
Picha hizo zinaonesha watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi hilo wakiwa kwenye karakana fulani wakitengeneza silaha zenye uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa.
Picha hizo zinaaminika kuwa zilipigwa katika jimbo la Borno nchini Nigeria.
Wachunguzi wanasema kuwa picha hizo zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama (Government Technical College Bama (GTCB).
Haijabainika iwapo mashine hizo za chuo hicho anuai zilinaswa na maafisa wa jeshi la Nigeria au la.
Hata hivyo Bama ni moja ya miji iliyokombolewa na jeshi la Nigeria.
Licha ya waasi hao kupigwa na kuondolewa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa Nigeria kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi ambayo yamewaacha wa Nigeria wengi wakishangaa wanakotoa silaha hizo kali.
Huu ndio ushahidi wa kwanza kuwa kundi hilo linauwezo wa kutengeneza silaha kali.(CHANZO BBC.COM)
Post a Comment
Post a Comment