Mchezaji wa Mbeya City Joseph Mahundi akilia baada ya timu yake kufungwa kwenye mchezo kati ya timu hiyo na Simba ya Jijini Dar es salaam |
Benchi la Simba |
Benchi la Mbeya City |
Patashika langoni mwa Simba |
Kocha wa Mbeya City Majao Mingange |
LIGI kuu ya Vodacom imeendelea leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine ulipozikutanisha timu za Mbeya City na Simba ya Dar es salaam ambapo kwa mara ya kwanza imevunja mwiko na kuichapa Mbeya City bao 1-0.
Tangu timu ya Mbeya City ipande daraja mwaka juzi haijawahi kufungwa na Simba katika uwanja wake wa nyumbani na mara ambapo katika msimu uliopita Simba ilifungwa nyumbani na ugenini.
Goli la kuvunja mwiko la Simba lilipatikana dakika ya 2 ya mchezo ambalo lilifungwa na Murshid Juuko kwa kichwa baada kona iliyopigwa na Mohamed Husein ambapo mpira ulitua kichwani kwa Murshid na kuusindikiza wavuni huku golikipa wa Mbeya City Juma Kaseja akichupa bila mafanikio.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Simba walikuwa kifua mbele kwa bao 1-0.Kipindi cha pili kwa timu ya Mbeya City kuonesha makeke langoni mwa Simba lakini washambuliaji wa timu hiyo walikosa ushirikiano na hivyo kujikuta wakishindwa kuliona lango la Simba.
Walinzi wa Simba Hassan Ramadhan, Said Hamis,Mwinyi Kazimoto, Justice Majabvi alijitahidi kuondosha hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwa timu yao ambapo washambuliaji wa Mbeya City Hamad Kibopile,Christian Sembuli, Themi Felix, Geofrey Mlawa na Rafael Alpha walionekana kukwaa kizingiti.
Hadi kipyenga cha dakika tisini kinapulizwa Simba walitoka kifua mbele kwa bao 1-0.
Baadhi ya wapenzi na mashabiki wa timu ya Mbeya City wamedai kuwa kocha mpya wa Mbeya City Majao Mingange ana kazi ngumu ya kurejesha hamasa za wachezaji wake hasa baada aliyekuwa kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi kuhamia timu ya Yanga.
Kocha Mwingange ambaye awali alikuwa akikinoa kikosi cha Ndanda ya Mtwara alisema kuwa kazi aliyonayo si kubwa sana kwa wachezaji wake na kuwa yapo marekebisho madogo ambayo yakifanyiwa kazi wachezaji hao wataonesha kabumbu safi katika michezo ijayo.
Post a Comment
Post a Comment