Baadhi ya abiria wa Basi la Newforce walioibua tafrani kwenye Kituo cha Mzani Uyole jana asubuhi |
Add caption |
Basi la Newforce likiwa katika kituo cha mizani Uyole jana |
Kituo cha Mizani Uyole jijini Mbeya |
Moja ya gari likishindwa kupita kwenye mizani ya Uyole baada ya kuwekewa mawe na abiria wa Basi la New Force |
Kipimo cha Mzani wa Uyole kikisomeka 3500 baada ya shinikizo la kurudia kupima mara ya pili ambapo awali ilisomeka 7750 |
Msimamizi wa kituo cha Mizani Uyole ambaye aligoma kuwaonesha kipimo wafanyakazi wa Basi la New Force ambao walidai kipimo kilichoelezwa na msimamizi huyo hakisemi ukweli |
ABIRIA
waliokuwa wakisafiri na Basi la Newforce lenye namba za usajili T 520 CXE
linalofanya safari kati ya Kyela na Dar es salaam walilazimika kuweka mawe
kwenye kituo cha mizani Uyole wakipinga kitendo cha wafanyakazi wa kituo hicho
kulitoza faini basi hilo kwa madai ya kuzidi uzito
Waliibua
tafrani wakionekana wakiwa na hasira wakibeba mawe na kuyaweka kwenye njia ya
kupita kwenye mizani ili kuzuia magari mengine yasipime kwa kile walichodai hadi
hapo watakapooneshwa uzito unaodaiwa kuzidi wa Basi hilo.
‘’Tunataka
watuoneshe uzito wa hii gari wanadai limezidi uzito wakati ndani ya Basi tupo
abiria 41 na hili basi linabeba abiria 57,’’alisema mmoja wa abiria
aliyejitambulisha kwa jina la Angelina Basiku anayesafiri kuelekea jijini Dar
es salaam.
Naye abiria
aliyejitambulisha kwa jina la Ephraim Mwankenja alisema kuwa kitendo hicho ni
wizi wa wazi wa baadhi ya watumishi wa mizani katika maeneo mengi ambao hutoza
faini kinyume cha taratibu.
Mwankenja
alisema iwapo Basi linakuwa limezidisha abiria au mizigo uzito wake unaonekana
na kuwa kitendo cha kusema Basi hilo
limezidi uzito wakati lina abiria wachache na halina mizigo ni kitendo
kinachotia mashaka utendaji wa wafanyakazi hao.
Hata hivyo alisema
kuwa kitendo hicho mbali ya kuwa na dalili ya wizi wa wazi pia kinaleta kero na
usumbufu kwa abiria wanaohitaji kusafiri kwa usalama.
Abiria
mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mwalukuta alisema kuwa yeye amekuwa
anasafiri mara nyingi na magari kuelekea Dar es salaam na kuwa iwapo Basi
limebeba mizigo mingi au kuzidisha abiria uzito huongezeka kwenye mizani na
kwamba ndani ya basi hilo siti nyingi ziko wazi.
Mkazi wa
Uyole aliyejitambulisha kwa jina la Michael Somo alidai kuwa kituo hicho cha
Mizani kimekuwa kikilalamikiwa na madereva wengi ambapo limekuwa ni tatizo sugu
kutokana na tabia ya kuongeza vipimo vya mizani kwa nia ya kujipatia fedha kwa
njia isiyo halali.
‘’Inawezekana
huu ndio utaratibu wanaoutumia hawa wafanyakazi kujipatia fedha kwa njia isiyo
halali, gari likizidi uzito linatakiwa kulipa fidia, gari letu ni tupu halina
abiria huo uzito umetoka wapi,’’alihoji kondakta wa Basi hilo aliyejitambulisha
kwa jina la Abdul Paresh.
Paresh
alisema kawaida uzito wa basi hilo unatakiwa usizidi GVM 23,000 na kuwa wafanyakazi wa mizani walipima uzito
ambao ulikuwa mbele ni GVM 8,550 na nyuma GVM 11,100 na hivyo kutakiwa kulipa
faini sh. 36,000 na kwamba hata hivyo walipofika kituo cha Makambako wamepima
tena uzito ambao umesomeka mbele GVM 7,400 na nyuma GVM 11,100.
Kwa upande
wake Yuhai Chen ambaye ni msimamizi wa mabasi ya New Force Nyanda za Juu kusini
alisema kuwa Basi hilo hata kama lingekuwa na abiria 61 bado uzito usingeweza
kuongezeka na kuwa kilichofanyika ni ujanja wa wafanyakazi hao kujipatia fedha
kwa njia isiyo halali.
Chen aliomba
ipimwe tena wafanyakazi wakakataa na kudai kuwa kompyuta yao ilikuwa mbovu na
kuhoji kuwa iwapo kompyuta yao ni mbovu inakuwaje wanatoa huduma.
‘’Huu ni
ubabaishaji wametupimia wanakataa kurudia kutupimia wakidai kuwa kompyuta ni
mbovu, inawezekana wanaibia watu kwa kutoa huduma kwa kompyuta mbovu’’alisema
Chen.
Msimamizi wa
kituo cha Uyole alipoulizwa tatizo hilo alisema kuwa yeye hana mamlaka ya kutoa
maelezo juu ya suala hilo kwa kuwa si msemaji wa TANROAD ambapo Mkuu wa
wahandisi wa TANROAD ambaye jina lake limesomeka kupitia namba yake ya simu ya
mkononi jina la Boniface Mkumbo alidai kuwa yupo njiani kufika eneo la kituo.
Basi hilo
liliondoka majira ya saa 5:00 katika kituo hicho cha Mizani Uyole bila masharti
ambapo pia Mkuu wa wahandisi wa TANROAD Mkumbo
alikuwa bado kufika eneo hilo kutolea ufafanuzi tatizo la wafanyakazi wa kituo
hicho kudaiwa kuzidisha vipimo vya uzito wa magari eneo hilo.
Hata hivyo
kwa mujibu wa Kondakta aliyesafiri na Basi hilo kuelekea jijini Dar es salaam
Abul Paresh alisema kuwa waliruhusiwa kuondoka hapo baada ya shinikizo la
abiria kutaka kurudia kupima Basi hilo ambalo katika kipimo cha kwanza
lililonekana limezidi 8,550 na nyuma 11,000.
Alisema
uzito huo haukuwiana na mzigo wa Basi hilo na kuwa baada ya kuondoka walipima
tena katika mzani wa Makambako ambapo wamepata uzito wa 7,400 mbele na nyuma
11,100.
Awali
walipotakiwa kupima tena walikataa na kuwa wamekwisha pima inatakiwa kulipa
faini hadi pale alipofika askari na mwandishi wa habari hizi ndipo walipopima
na kukuta uzito wa GVM 7,750 na nyuma GVM 11,000.
Post a Comment
Post a Comment