KAZIMOTO KUPANDISHWA
KIZIMBANI
KIUNGO wa Simba Mwinyi
Kazimoto anasubiri kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumshambulia na
kumpiga mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Mwanahiba
Richard.
Kazimoto alifikishwa
polisi jana ana kutakiwa kuripoti leo mchana ambapo alichukuliwa maelezo yake,
upepelezi umeanza kwa ajili ya kupandishwa kizimbani.
Shirikisho la soka
nchini TFF linasubiriwa kutoa tamko juu ya sakata hilo na kwamba iwapo Kazimoto
atapatikana na hatia adhabu ya juu ni kufungiwa kucheza soka kwa muda wa mwaka
mmoja.
Mwanahiba alipatiwa
matibabu hospitali ya Mkoa Shinyanga na sasa anaendelea vizuri ambapo kampuni
ya Mwananchi imetoa tamko la kulaani kitendo hicho.
Post a Comment
Post a Comment