Mwandishi wa MwanaSpoti Mwanahiba Richard anayedai kupigwa na Mwinyi Kazimoto |
Mchezaji wa Simba anayedaiwa kumpiga mwandishi wa habari wa MwanaSpoti |
Mchezaji wa Simba Mwinyi
Kazimoto amefikishwa kituo kikuu cha polisi mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za
kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la MwanaSpoti Mwanahiba Richard.
Kazimoto anayedaiwa
kufanya kosa hilo kutokana na kudai kuwa mwandishi huyo aliwaandika vibaya kuwa
wachezaji wa Simba waliocheza mechi ya Prisons na Mbeya City walikuwa chini ya
kiwango na wanapaswa wachunguzwe kwa maana ya kuwa wamepewa rushwa.
Akizungumza juu ya
tukio hilo kama alivyokuwa akizungumza na kituo kimoja cha redio usiku huu
Mwanahiba alikuwa na haya ya kusema;
''Stori hiyo mie
niliandika mwaka jana,..kuna siku alinipigia simu akaniuliza ni nani amekupa
hiyo stori, nikamwambia siwezi kumwambia
aliyenipa stori
akaanza kunitukana kwenye simu,
Jana tulipokuwa uwanja
wa kambarage wakati tunamfuata kocha akanifuata na kuniuliza wewe ndiye
Mwanahiba nikamjibu ndiyo akasema unakumbuka niliwahi kukupigia simu
nikamwambia ndio akasema mbona hujaniambia aliyekupa hiyo stori?
Nikamjibu mie sina
mamlaka ya kukutajia aliyenipa hiyo stori nilishaipeleka gazetini na ikatumika
akaniuliza sasa unaamua nini, nikamjibu mie sina la kuamua, akasema sasa yeye
anaamua akaanza kunitukana na kunipiga...mie nikaamua kwenda polisi, hivyo
ndivyo ilivyokuwa"...SAYZ MWANAHIBA
Post a Comment
Post a Comment