Ads (728x90)

Kikosi cha timu ya Prison kilichochuana na timu ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine Jumapili na kutoka suluihu ya bila kufungana

Kikosi cha timu ya Mbeya City kilichokwaana na timu ya Prison mzunguko wa pili timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0

Wachezaji wa akiba wa timu ya Prison walipocheza na timu ya Mbeya City uwanja wa sokoine Jumapili


Benchi la ufundi la timu ya Prison

Benchi la Ufundi la timu ya Mbeya City


Kama ilivyo ada vijembe vya mashabiki havikukosekana

Basi la Timu ya Prison

Basi la timu ya Mbeya City



Tofauti na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma mara baada ya timu ya Mbeya City kupanda daraja kucheza ligi kuu ya Vodacom mwaka 2013, hamasa za timu hiyo iliyokuwa chini ya kocha Juma Mwambusi ililiamsha Jiji la Mbeya na nchi nzima ilikuwa kila kona Jina la Mbeya City lilikuwa kinywani mwa mashabiki.

Mashabiki lukuki kutoka kila kona ya Jiji la Mbeya na mikoa ya jirani walihamasika kuishabikia timu hiyo ambayo mwishoni mwa ligi hiyo walishikilia nafasi ya nne wakiwa nyuma ya wababe wa soka nchini, Azam, Yanga na Simba.

Nyota ya vijana hao wanaotoka katika Jiji lenye mandhari ya  Kijani kibichi iliendelea kuwaka na hata kusahau kuwa kulikuwa na timu nyingine iliyopo mkoa wa Mbeya timu ya Maafabde wa Magereza Prison ambao kwa kipindi hicho ilikuwa almanusura itelemke daraja.

Katika msimu huu wa ligi raundi ya kwanza Prison ilipokutana na Mbeya City waliitandika bao 1-0 na hivyo kufuta uteja  uliodumu kwa takribani msimu mzima uliopita ambapo Prison ilikuwa ni wateja wa Mbeya City kila walipokutana.

Katika mchezo wa leo ilitarajiwa Mbeya Cityb wangeweza kulipiza kisasi cha kufungwa katika mzunguko wa kwanza, hali haikuwa hivyo, timu zote zikicheza kwa kukamiana na kutegeana katika kipindi cha kwanza hakuna iliyoona lango la mwenzake.

Kipindi cha kwanza cha mchezo timu ya Prison ambayo juma lililopita iliwatoa kamasi wababe wa ligi hii Yanga ya Dar es salaam kwa kuipigisha kwata na kuponea chupuchupu ya kufungwa, leo iliingia huku mashabiki wakiwa na ari kubwa ya kuona umahiri wa wachezaji hao wa Prison wakiikimbiza Mbeya City ambayo kwa msimu huu imeonekana ikifanya vibaya katika ligi hiyo.

Dakika za mwanzo za mchezo huo Prison ilionekana ikiutawala zaidi mpira kuliko wapinzani wao Mbeya City ambapo wachezaji  Jumanne E;lfadhil, Freddy Chudu, Jeremia Juma na Mophamed Mkopi walionekana kuisumbua sana ngome ya Mbeya City iliyoongozwa na Deo Julius mchezaji wa zamani wa Mbeya City aliyeachwa na kuhamia Kagera Sugar kabla ya kusajiliwa tena kwenye dirisha dogo na Mbeya City.

Deo alionekana kuokoa michomo mingi iliyoelekezwa golini kwa Mbeya City huku mara kadhaa walinzi wa City akina  Haruna Shamte,Hassan Mwasapili,Tumba Lui na Kenny Ally wakiwa wametoka na kumuacha golikipa Juma Kaseja pekee golini.

Kipindi cha pili kilianza huku kila timu ikionesha uchu wa kufunga lakini hata hivyo bahati haikuwa kwa pande zote mbili ambapo mara kadhaa wachezaji wa timu zote walionekana wakichezeana rafu za hapa na pale hali iliyoanza kuonesha wachezaji hao kama wamechoka ama wameanza kukosa umakini katika kumiliki kabumbu.

Ilikuwa ni dakika ya 72 ya mchezo amba;po ilipigwa kona na Juma Seif Kijiko wa Prison na kutaka kutinga wavuni huku Hassan Mwasapili  akiuokoa mchomo huo wakati Juma Kaseja alikuwa amekwisha utema mpira na baadaye Salum Kimenya wa Prison kuusindikiza mpira wavuni ambapo mshika kibendera wa kushoto alinyoosha juu kibendera chake kuashirikia kuwa alikuwa ameotea.

Mbali na timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana lakini mashambulizi ya timu zote kwa kila upande yalizaa kona 10 ambapo kila timu ilipata kona 5 wakati mchezaji wa Prison Benjamin Asukile alizawadiwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya  

Post a Comment

Post a Comment