Ads (728x90)

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     





















MWENYEKITI wa
Kamati ya  Usalama Barabarani
Mkoa wa Mbeya,Allan
Mwaigaga(Mwaji) amesema kuwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais
John Magufuli
katika kipindi cha siku 100 alizokaa madarakani zimewaumbua
wakwepa kodi
wakubwa na wananchi waliokuwa wakiishi maisha
bandia.

Mwaigaga
anayemiliki Kampuni ya Mwaji Group alisema
juzi jioni alipotembelea  Makao
Makuu ya
Ofisi ya Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania
(TAJATI) zilizopo
jijini Mbeya muda mfupi akitokea jijini Dar es
salaam.

Akizungumza na
Waandishi hao alisema kuwa ameamua
kutumia fursa hiyo kuwaomba watanzania waliokuwa wakifanya
biashara zao
kiujanja ujanja na kukwepa kulipa kodi kwa makusudi kuwa
sasa ni muda wao wa
kutubu ili uchumi wan chi uweze kupaa. 

“Kama tulifanya
kosa la kukwepa kulipa kodi ambazo
ndizo zinazotegemewa na serikali kuboresha huduma za
kijamii,basi wote
tutubu,tumuombe Mungu atusamehe kwa kufanya kosa hilo  baya na ndio lililoifanya nchi yetu
iendelee
kuwa masikini” alisema Mwaji. 

Kuwa ili uchumi
wa nchi uweze kuendelea  kwa kasi
ni wajibu wa kila mwananchi asimame
kidete na kuunga mkono jitihada za Rais wa awamu ya tano
zinazofanywa na
Magufuli ili kuhakikisha kuwa heshima ya nchi iliyotoweka
katika usimamizi wa
fedha za umma inarudi. 

Alisema kuwa nchi
zilizoendelea zinawashangaa
watanzania walioshiriki kuua uchumi wao na kukimbilia kuomba
misaada nje  wakati kazi kubwa
iliyofanywa na muasisi wa
Taifa hili,Baba wa Taifa,Julius Nyerere(Hayati) kujenga kila
kitu lakini ni
watanzania wenyewe ndio walioua uchumi
wao.

Alihoji idadi ya
viwanda vilivyokufa,mashirika ya umma
na kampuni zilizohujumiwa na kufa,mashamba makubwa ya
umma,miundombinu ya reli
na kudai kwamba kama angeruhusiwa yupo tayari na wadau
wenzake kumiliki Reli ya
Tazara na kuwaondoa wote waliohusika ili kazi ianze
upya.

“Kati ya siku
80 nilizokaa Dar es salaam katika
kipindi cha siku 100 za Rais Magufuli watu waliokuwa wapiga
mizinga jijini Dar
es salaam sasa hawapo na hawaonekani kwenye mabaa na kumbi
za starehe,sasa
hawana kitu hata magari wanayomiliki watauza,subirini
kununua gari kwa milioni
mbili” alisema Mwaji. 

Alisema kuwa
watanzania wengi waliojipatia fedha kwa
njia haramu kufanya biashara chafu na kushindwa kulipa kodi
waliamua kuishi
maisha bandia ili waonekane tofauti na wananchi wengine
ambao hawana kitu ndipo
hapo nchi ilipofikishwa ikiwa haina
nidhamu. 

Akizungumzia
sekta ya Utalii na Uwekezaji katika mikoa
ya kanda ya nyanda za juu kusini,Mwaji ambaye anajipambanua
kuwa ni
Mjasiriamali wa kati aliwashauri 
Wana
TAJATI kuhakikisha kuwa wanatumia vyema taaluma yao ya
habari ili kuisaidia
serikali iweze kufikia malengo yake ya kukuza uchumi katika
mikoa hiyo. 

Alisema sekta ya
utalii imepewa kipaumbele zaidi
kwenye mikoa ya Kaskazini tofauti na mikoa ya kusini,hivyo
ni jukumu la chama
hicho kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na hiyo ni kazi ya
wanahabari
kutangaza utalii na kushiriki kwa vitendo kuibua na
kutembelea hifadhi zilizopo
kuliko kusubiri watalii kutoka 
nje ya
nchi. 

Kwa upande wa
sekta ya barabara na miundombinu
yake,Mwenyekiti huyo wa Usalama barabarani mkoa wa
Mbeya,alisema kuwa serikali
ina changamoto kubwa ya kuboresha barabara kuu inayotoka
Uwanja wa ndege wa
Songwe hadi eneo la Uyole umbali wa kilometa
40. 

“Barabara
kutoka uwanja wa ndege wa Songwe hadi jijini
Mbeya isipopanuliwa mapema ni shida,nimeshuka uwanja wa
ndege,kabla sijafika
Mwanjelwa ndege tuliyopanda inatua Dar,zaidi ya masaa mawili
tulikuwa kwenye
foleni,magari ni mengi na barabara kuu ni moja” alisema
Mwaji.
 Alisema
anaamini kasi inayoonyeshwa na Rais Magufuli ienee nchi
nzima kwa kuwa fedha
zaidi ya Sh bilioni 4 alizozizuia kwa ajili ya sherehe za
uhuru zimefanya kazi
kubwa ya ujenzi wa barabara ya Mwenge jijini Dar es salaam
na kwamba anapaswa
kuutupia macho uwanja wa Songwe wenye uwezo wa ndege kubwa
kutua na kupungua
kwa nauli .

 

Post a Comment

Post a Comment