Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipotembelea Ofisi za TAJATI jana asubuhi |
Waziri Nape akionesha eneo la jengo la Ofisi za TAJATI ambalo chama hicho kimewdeka mpango wa kuwa na chumba cha Habari chenye studio kubwa ya kisasa |
Waziri wa
Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye amewapongeza wanahabari wa Chama
Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) na kuwataka
kukitangaza chama hicho nchi nzima ili kilete tija na manufaa kwa Taifa.
Waziri Nape
alisema hayo jana alipozuru ofisi za TAJATI Jijini Mbeya na kusema kuwa fursa
ya wanahabari kuandika habari za Utalii na Uwekezaji ni kubwa hivyo ni vyema
chama hicho kikasambaa nchi nzima ili fursa hiyo iwafikie wananchi wengi.
‘’Kisambazeni
chama chenu nchi nzima, serikali itatoa ushirikiano kwenu, andikeni habari za
Utalii na Uwekezaji ili vivutio vya Utalii vitambulike na fursa za uwekezaji
zijulikane,’’alisema Waziri Nape.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili alisema kuwa kuanzishwa kwa chama
hicho kumelenga kuibua fursa za utalii na uwekezaji zilizopo nchini na
kuzitangaza ili vitambulike ndani na nje ya nchi.
Awali Waziri
Nape alitembezwa kwenye ofisi za TAJATI na kuelekezwa mikakati ya chama hicho
kulifanya jengo hilo kuwa lenye chumba cha Habari na studio ya kisasa
itakayowawezesha wanahabari kupata taarifa mbalimbali za Utalii na uwekezaji.
‘’Tumelenga
kuwa na chumba cha Habari na Studio ya kisasa itakayowawezesha wanahabari
kupata fursa za habari za Utalii na Uwekezaji nchini,’’alisema Christopher
Nyenyembe Makamu Mwenyekiti wa TAJATI.
Post a Comment
Post a Comment