Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiangalia ujenzi wa Meli za abiria bandari ya Itungi wilayani Kyela leo mchana |
Sehemu ya Ufukwe wa Ziwa Nyasa Bandari ya Itungi wilayani Kyela |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akioneshwa eneo la ujenzi wa meli bandari ya Itungi wilayani Kyela leo mchana |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos
Makalla amemwagiza mkandarasi kampuni ya
Songioro Marine kukamilisha ujenzi wa meli 3 za Abiria ambazo zinajengwa na
kampuni hiyo kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa Mkuu
huyo wa Mkoa amesema kuwa mara baada ya kutembelea Bandari ya Itungi(Itungi
Port) iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya ameridhishwa na muendelezo wa ujenzi
wa meli hizo ambapo meli ya kwanza inatarajiwa kumalizika Agosti Mwaka huu.
Alisema Meli hiyo
itakuwa na uwezo kubeba abiria 200 na tani 200 pamoja na magari 10-15.
‘’Meli ya pili yenye
uwezo wa kubeba tani 1000 za mizigo ambapo meli ya tatu ambayo pia ina uwezo wa
kubeba tani 1000 inatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2017,’’alisema Makalla.
Amefafanua kuwa
kukamilika kwa meli hizo kutarahisisha usafiri kwa mikoa inayopakana na Ziwa Nyasa
ambayo ni Mbeya(Kyela)Njombe(Ludewa)Ruvuma(Nyasa) na nchi jirani za Malawi na
Msumbiji ambapo wananchi watanufaika kibiashara kati ya nchi hizo.
Aidha ameahidi kutoa ushirikiano wa
dhati na Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha barabara ya km 6 ya Itungi kuelekea Njiapanda
Kiwira itajengwa kwa kiwango cha lami ili bandari hiyo ifikike kiurahisi.
Mheshimiwa
Makalla pia amezitaka ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mbeya(RAS),DC na Menejimenti ya
Bandari kuitangaza Bandari ya Itungi ili wananchi wazitambue fursa zilizopo
ndani na nje ya nchi.
Post a Comment
Post a Comment