Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiagiza kupunguzwa kwa gharama za upangaji wa soko la Mwanjelwa alipotembelea jana kufuatilia maagizo aliyoyatoa kwa watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munassa alipotembelea soko jipya la Mwanjelwa jana. |
MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amekonga nyoyo za
wafanyabiashara na wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuagiza kupunguza gharama za
upangaji katika vizimba vya soko hilo jipya la Mwanjelwa kutoka Sh.500,000 hadi
sh 350,000.
Maagizo hayo ameyatoa mara alipotembelea kwa mara ya pili
soko hilo kwa nia ya kufuatilia maagizo aliyoyatoa katikati ya wiki sokoni hapo
ikiwa ni pamoja na kutowapangisha wafanyabiashara kwenye eneo la dampo la
takataka.
Huku akishangiliwa na wafanyabiashara wa soko hilo Makalla
pia aliagiza vizimba vyote vilivyopo nje ya soko hilo kulipiwa sh. 1000 kwa
siku sawa n ash. 30,000 kwa mwezi badala ya sh. 90,000 inayolipwa sasa.
Ametoa wito kwa wafanyabiashara kufika sokoni hapo na kuomba
vizimba na maduka na kutoa ofa ya mwezi mmoja wa Mei kutolipia kodi ili kutoa
unafuu kwa wananchi na kuongeza wapangaji.
Post a Comment
Post a Comment