RC MBEYA ALA CHAKULA NA WAFUNGWA GEREZANI
MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla aibukia kwenye Gereza la
Mahabusu la Ruanda lililopo Jijini Mbeya na kula chakula pamoja na wafungwa
gerezani.
Pamoja na kula chakula na wafungwa Makalla pia alikagua
malazi ya wafungwa pamoja na zahanati ambapo pia amewaahidi wafungwa na
mahabusu kufuatilia tatizo la ucheleweshaji wa kesi kutokana na kisingizio kwa
kuchelewa kwa majalada ya upelelezi.
Mbali na kutembelea wafungwa na mahabusu gerezani,Makalla
ametekeleza ahadi yake ya kuitembelea timu ya Prison kama alivyofanya kwa timu
ya Mbeya City na kukabidhiwa jezi ya timu hiyo na kutoa wito kwa timu zote za
Prison na Mbeya City kuendelea kufanya vyema katika ligi Kuu ili ziendelee
kutoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya msimu ujao.
Post a Comment
Post a Comment