Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akitembelea soko jipya la Mwanjelwa jana |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara alipotembelea soko jipya la Mwanjelwa jana |
Mkuu wa mkoa
wa MBEYA Amos Makalla jana ametembelea soko jipya la Mwanjelwa na kutoa maagizo
mazito baada ya kutoridhishwa na taarifa za uendeshaji wa soko hilo.
Katika ziara
yake Makalla alibaini gharama kuba ya kodi ya upangaji ambayo inaonekana
kutoendana kipato halisi cha wafanyabiashara na hivyo kuwaagiza Halmashauri ya
Jiji la Mbeya kukaa meza moja na wakopeshaji Benki ya CRDB ili kuangalia
uwezekano wa kuwapunguzia kodi wafanyabiashara wa soko hilo.
Kadhalika
amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU)
ashirikiane na Ofisi ya Usalama wa Taifa kufanyia uchunguzi suala hilo ndani ya
mwezi mmoja kuchunguza mchakato mzima wa ujenzi ulivyofanyika.
Post a Comment
Post a Comment