Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amoss Makalla akiwa ndani ya jezi ya timu ya Mbeya City |
Kapteni wa
timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Amos
Gabriel Makalla ametua kwenye timu za soka zinazocheza Ligi Kuu zilizopo Jijini
Mbeya,Prison na Mbeya City na kuwataka
viongozi wa timu hizo kumtumia vyema ili kuupa heshima mkoa wa Mbeya.
Makalla
ambaye ndiye Mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa sasa alipata kuiongoza timu ya bunge kwa
mafanikio makubwa kwa kipindi chote cha miaka 10 aliyekuwepo bungeni na kusema kuwa
atatumia mbinu na uzoefu wake katika
medani ya soka kuhakikisha timu hizo zinafanya kwa mafanikio katika mechi
zilizosalia.
‘’ Ee Mola
wangu kwa niaba ya Wanambeya naziombea ushindi timu za mkoa wa Mbeya, Prison na
Mbeya City ili ziweze kubaki ligi kuu, nawaomba wakazi wote wa mkoa wa Mbeya
tushirikiane ili kuzipa sapoti timu zetu,’’alisema RC Makalla.
Mheshimiwa
Makalla pia alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa timu ya Prison kumpatia
jezi ya timu hiyo kwa kuwa yeye ni mlezi wa timu zote mbili za mkoa wa Mbeya.
‘’Mimi ni
mlezi wa timu za madaraja yote mkoa wa Mbeya, naombeni ushirikiano wenu,
Viongozi wa Prison naombeni jezi ya timu yenu,’’alisema Makalla.
Hivi
karibuni viongozi wa timu ya Mbeya City walitumia fursa yao ya kukutana na Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na kumkabidhi jezi ya timu hiyo.
Post a Comment
Post a Comment