Ads (728x90)




Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa wanaosubiri huduma kwenye hospitali ya wazazi Meta Jijini Mbeya leo asubuhi





MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo amefanya ziara kwenye Hospitali ya wazazi Meta na kuagiza kuchukuliwa hatua kali kwa muuguzi aliyemtolea lugha chafu mzazi Salome Swaya ambaye alijifungua hospitalini hapo hivi karibuni.
 
Makalla ametoa siku 7 kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya wazazi ambayo iko chini ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo ameunda tume ya watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa  Hospitali hiyo kuchukua kufanya uchunguzi na kuchukua hatua.

Tume ya watu wanne iliyoundwa kufuatilia tuhuma hizo inamhusisha Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Matroni, Patroni na Mjumbe mmoja kutoka Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya.

Makalla alisema lengo la kuundwa kwa tume hiyo ni kwa ajili ya kupata ukweli juu ya kutolewa kwa lugha chafu kwa mgonjwa huyo ikiwa ni pamoja na kupata upande wa pili wa Muuguzi aliyetuhumiwa ambaye hakuwepo hospitalini hapo wakati wa ziara yake.

Sanjari na tukio hilo Mheshimiwa Makalla amekutana na kero ya msongamano wa wagonjwa mawodini hali ambayo imesababisha baadhi ya wagonjwa kukosa vitanda na wengine kulala kitanda kimoja zaidi ya mtu mmoja.

‘’Nawaomba madaktari na wauguzi, fanyeni kazi kwa kuzingatia maadili wakati mnapotekeleza majukumu yenu.

Aidha Mheshimiwa Makalla amesema kuwa atafuatilia wizara ya Afya ombi la ujenzi wa wodi ya wazazi ambayo ni dhamana ya mkopo kutoka hazina fedha ambazo hospitali hiyo iliomba hapo awali.

Post a Comment

Post a Comment