Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na watafiti wa kituo cha Utafiti wa Kilimo na Mifugo Uyole |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa katika kundi la Ng'ombe wanaofugwa kwenye shamba la Mifugo la la kituo cha Utafiti Uyole |
Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya Amos Makalla ametoa somo kwa taasisi za utafiti wa kilimo, mifugo wa
chuo cha kilimo Uyole akiwataka kuwekeza zaidi kwenye utafiti ili kutoa wataalaam bora wa kilimo na ufugaji.
Makalla
amesema ili kujitosheleza kwa chakula na mazao ya mifugo nchini wataalamu bora wa
utafiti wanahitajika ikiwa ni pamoja na kuwa na malighafi ya Viwanda.
Amesema Rais
Dkt John Pombe Magufuli anataka nchi iwe na viwanda vidogo, viwanda vya Kati na
vikubwa na kwamba viwanda hivyo vitategemea zaidi malighafi za ndani ambazo
zitatokana na kilimo cha kitaalamu sanjari na upatikanaji wa pembejeo bora za
kilimo.
Amefafanua
kuwa nchi yoyote inayowekeza kwenye utafiti huondokana na matatizo ya kukosekana
kwa mbegu bora za mazao ya kilimo na mifugo na hivyo jambo pekee la taasisi za
Uyole kutumia teknolojia ya kisasa kwa usindikaji wa mazao ili kuyaongezea
thamani.
Kadhalika Makalla amewataka maofisa kilimo,vikundi vya wakulima na wafugaji
kutembelea chuo cha Utafiti Uyole ili kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo na
ufugaji ili kuzalisha kwa tija.
Post a Comment
Post a Comment