Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa na wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni |
Mkuu mpya wa wilaya ya Chunya Rehema Manase akila kiapo cha utii mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla |
Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia Undalusyege Kitta akitia saini kwenye fomu ya kiapo mara baada ya kula kiapo cha utii na utumishi wa serikali mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla |
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chalya Julius Nyangindu akila kiapo cha utii serikalini mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla. |
Mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akila kiapo cha utii serikalini mbele ya aMkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla. |
Mkuu wa wilaya ya Mbarali Reuben Ndiza Mfune akitia saini kwenye fomu ya kiapo baada ya kula kiapo cha utii na utumishi serikalini mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla |
MKUU wa mkoa
wa Mbeya Amos Makalla amewataka wakuu wapya wa wilaya kuifanya serikali kuwa
rafiki na wananchi ili kusaidia kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii
kwenye maeneo yao.
Makalla
aliyasema hayo wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Mbeya ambao
waliteuliwa hivi karibuni na Rais John Pombe Magufuli.
‘’Falsafa
yangu ni kuwa na serikali rafiki na wananchi,Ofisi za serikali ziwe kimbilio la
wananchi, msizifanye za serikali kuwa kama kituo cha polisi,’’alisema Makalla.
Alisema
katika utendaji wake amekuwa na desturi ya kuwafuata wananchi na kusikiliza
matatizo yao ambapo amewataka wakuu hao wa wilaya nao waendelezea desturi hiyo
ambayo ndiyo inayosaidia uwajibikaji wa serikali kwa wananchi wake.
‘’Wananchi wanazo
kero nyingi, kusikiliza kero za wananchi ndio kipimo chenu cha uwajibikaji,
kasikilizeni kero za wananchi zile zitakazowashinda zileteni kwangu kwa
maandishi zinifikie Jumatatu asubuhi,’’alifafanua.
Alisema si
vyema kuwaacha wananchi wabaki na manung’uniko kwa kuwa kufanya hivyo
kunawajengea chuki na serikali yao na hivyo kupunguza uwajibikaji na kasi ya
maendeleo ya wananchi.
Aidha
Makalla ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya
aliliagiza Jeshi la Polisi kupambana vikali na majambazi wanaotumia silaha kwa
kuwa hao wamekuwa wakiwajengea hofu na hata kuwaua raia wasio na hatia.
‘’Polisi
nawaagiza jambazi akija na moto na wewe na wewe nenda kwa moto,nendeni
mkapambane na majambazi, mjue kuwa jambazi mwenye silaha akikuwahi amekuua,
hivyo ili asiwahi kukuua muanze yeye hili litasaidia kuwamaliza majambazi,’’alisisitiza
Makalla.
Wakuu wa
wilaya walioapishwa na wilaya zao kwenye mabano ni pamoja na Rehema Manase
Madusa(Chunya),Claudia Undalusyege Kitta(Kyela)Chalya Julius Nyangindu(Rungwe)Reuben
Ndiza Mfune(Mbarali) na William Paul Ntinika(Mbeya).
Post a Comment
Post a Comment