Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) Agosti 8, 2016 |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na Waandishi wa Habari na kutoa taarifa za ujio wa Waziri Mkuu kwenye Ofisi za TAJATI leo asubuhi |
Mheshimiwa Makalla akisalimiana na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAJATI leo asubuhi |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ofisi za TAJATI leo asubuhi kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya Mariam Mtunguja |
Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe (kushoto)akielezea maudhui ya chama hicho mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya leo asubuhi |
Mwenyekiti wa TAJATI Taifa Ulimboka Mwakilili akimuonesha Mheshimiwa Makalla baadhi ya picha za kazi za wanatajati. |
Waziri mkuu
wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua
Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) Agosti,8,
2016.
Akitoa
taarifa hizo katika Ofisi za TAJATI leo asubuhi Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos
Makalla alisema amefurahishwa na malengo ya chama hicho kwa kuwa kitachangia
kuchochea Utalii na Uwekezaji nchini na kuwa uzinduzi wa chama hicho utafanywa
na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
‘’Tunamtarajia
Waziri Mkuu Agosti 8, wakati wa maonesho ya Kilimo kanda ya Nyanda za Juu, moja
ya kazi za mwanzo kuzifanya siku hiyo ni kuzindua Chama Cha Waandishi wa Habari
za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI)’’ alisema.
Mheshimiwa
Makalla ambaye aliyetumia fursa hiyo kufahamiana kwa karibu na wanaTAJATI
alisema kuwa chama hicho kina fursa ya kubwa ya kuibua na kutangaza Utalii na
Uwekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuwataka kushirikiana na Wizara ya Viwanda
na Biashara,kituo cha Uwekezaji(TIC), Wizara ya Maliasili na taasisi zake
ikiwemo Bodi ya Utalii na TANAPA.
"Mkishirikiana
vizuri na wizara hizo na taasisi zake na mkajitangaza nyinyi wenyewe na fursa
tulizonazo nina uhakika utalii na uwekezaji utaongezeka nchini’’alifafanua.
Ili
kujitangaza zaidi ndani na nje ya nchi Mheshimiwa Makalla aliwataka Wanatajati
kufungua website(wavuti) ambayo itasaidia kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa
na TAJATI na manufaa yake kwa Taifa.
Aidha
ameeleza kuwa moja ya shughuli alizopangiwa Waziri Mkuu mara atakapowasili
mkoani Mbeya siku ya tarehe 8/8/2016 ni kufanya
uzinduzi rasmi wa Chama hicho.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa TAJATI Taifa Ulimboka Mwakilili alisema kuwa chama hicho
kimeshafanya ziara za ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuibua na kutangaza
fursa za Utalii na Uwekezaji nchini hivyo ujio wa Waziri Mkuu utaibua hamasa kubwa
katika kufuatilia fursa za Utalii na Uwekezaji nchini.
Wakati huo
huo Mheshimiwa Makalla amezitaka
halmashauri za mikoa 7 ya nyanda za juu kusini , washiriki wa maonesho ya Nane
nane, wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha maonesho ya mwaka huu yanakuwa
ya dira na taswura ya kuigwa kwa maonesho
ya kanda zingine.
Akizungumza
kwenye kikao cha mwisho cha maandalizi ya maonesho hayo ambayo yanajumuisha
mikoa 7 ya Mbeya,Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma,Rukwa na Katavi, Mheshimiwa Makalla
alisema maonesho hayo yatazinduliwa na Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt.
Charles Tizeba na kufungwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Kwa upande
wake Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa mikoa hii ya Nyanda za
Juu Kusini ndiyo dira ya Kilimo na chakula kwa mikoa mingine nchini hivyo
anatarajia maonesho hayo yawe ya mfano kwa kanda zingine zenye maonesho ya aina
hiyo mwaka huu.
Post a Comment
Post a Comment