MAISHA ya watu wa kawaida maeneo mengi ya vijijini hukumbwa na misukosuko anuai ikiwemo kukosekana kwa huduma muhimu za afya,elimu,maji, nyumba bora za kuishi na mengineyo, hata hivyo jamii ya watu hao wa vjijini wanapofikia umri wa mzee kama huyu hushindwa kujimudu kimaisha hususani kutokana na mazingira waliyokulia.
Nyumba wanazoishi hazishabihiani na uimara wa aina yeyote ambazo zinaweza angalau kuhimili mikikimikiki hususani unapotokea uharibifu wa mazingira na ukataji miti ovyo usiozingatia usalama wa watu waishio katika nyumba hizo nyumba hizo utaziona zimejengwa na kuezekwa kwa nyasi.Aidha baadhi ya maeneo ya huko yamekumbwa na ukame huko vijijini kutokana na kukosekana kwa mvua katika msimu uliopita laiti kama kungekuwa na mipango na elimu madhubuti kwa wananchi wa maeneo hayo kuhifadhi mali asili za misitu bila kukata ovyo janga la ukame na njaa visingefika katika vijiji hivyo hivyo hulazimika kusafiri kwa mwendo mrefu kwa kutumia Punda kutoka kijiji kimoja hadi kingine kwa ajili ya kutafuta chakula.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kuna kazi sana,kuhusu usemi wako katika hoja husika.la muhimu hapa nijinsi ya kuangalia maisha binafsi ya mtu na mazingira yanayo mzunguka huko vijijini. nyumba ya matofari ya udongo/kuchomwa,na kuenzekwa kwa nyasi kwagu biafsi sioni ubaya,na wala siyo ndo umasikini.inabidi tubadilike mitizamo yetu kuhusu maisha ya kijijini kwa ujumla.ukiwa kijijini na kuwa mpembuzi sawasawa utagundua tatizo ninini mzee kama huyo kuwa katika hali kama hiyo.wakati jirani yake anaonekana yoko vizuri kimaisha.wengi vijijini ni wavivu,hawajitumi,napia kwa upande mwingine serikali nayo haisemi haiwakumbushi,haiwahamasishi,watu na maendeleo yao,kwa kufuatana na mazingira wanayo ishi. kaka s
ReplyDeleteNyumba ya tofari iliyojengwa kwa udongo bila saruji, wanamudu kuchoma tofari kwa kukata miti ambayo ni sehemu ya rasilimali zilizopo huko vijijini, muhimu ni kukumbushana katika uwajibikaji na ushirikishwaji
ReplyDelete