Ads (728x90)

Mara nyingi mwanadamu amekuwa akishindwa kukabiliana na mambo mbalimbali yanayomzunguka katika jamii kutokana kukosa kuhimili mikiki anuai ya maisha.

Lakini iwapo utatengeneza mambo yako kiufasaha ni matarajio kwamba hakuna tatizo lolote ambalo linaweza kukukabili ambalo linatokana na uwezo wa kibinadamu isipokuwa lile linalotegemea kudra za Mwenyezi Mungu.

Ni matumaini yangu kwamba kila mmoja anahitaji maisha bora yenye kila aina ya raha na starehe jambo ambalo aghalabu huwakuta wale wenye ukwasi wa maisha ilhali wenye ukta wakiishi katika dhiki na matarajio yasiyotimilivu.

Kwa kulijua hilo ni wajibu wa kila mwanadamu kujijengea mazingira fasaha ambayo yatamnufaisha katika dunia na kesho akhera kwa kujiandalia maisha yake hapa duniani ikiwa ni pamoja na kuishi vyema na jamii inayomzunguka.
wakatabahu...........
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

  1. karibu wa ufasaha tena kwa kutumia fasihi,kuna mwenzako barazani anaitwa Fatma naye yumo!,sasa kiswahili kinakua kwa kasi....nawahitaji zaidi watumiaji wa ngano za lugha na stahili za ushairi katika kukipa mshawasha na kuondoa tabaka la harara za semi mbovu za kiswahili.
    rambi rambi zangu kwako kwa kazi yako makini

    ReplyDelete
  2. Istilahi pana ya lugha adhimu inakwenda mkabala na matamshi ya watu kulinga na sehemu watokako,mathalani watu wa Mrima wana lahaja za kimrima ilhali watu wa pwani nao wana lahaja za kipwani, vila vile watu wa Pemba wana lahaja za kipemba,kadhalika na watu wa Mvita na wengine na wengine hivyo medani hii nadhani itatoa chachu kwa watumiaji mahiri wa lugha ya kiswahili kuboresha matamshi yao ili yasipoteze maana halisi ya lugha.

    Wakatabahu.

    ReplyDelete
  3. Nunu ni nani wa kununiwa, nunu nanena kwa nuni, iwe neno liso nunu, bali watumwa wa nuni na kalamu adhimu.

    Nunu, vije leo wanune, mibavu watunishane,waumiao wagune, kufanya siasa kidume.

    Nunu sisi tuna mavune, kuibiwa kuporwa kutiwa ndani, kisa muafaka kusaini?

    Nunu si mnunaji bali leo sitanuna uwazi nimebaini,uovu ulo ndani, madaraka kutamani, kamwe haki haipatikani, litendwalo ni dhuluma kubaka wari na wajane.

    Ai! askari wa bara kuvamia visiwani,kisa kulinda amani, iwapi imepotea?

    Bali kulinda maslahi ya wachache walobobea, rushwa ubabe na utawala wa mabavu unokosesha watu amani.

    Vije leo tujivune, ilhali watu waumizwa na kuwa kama wakimbizwa, kuacha majumba na wana, eti amani ipo iwaapi haki ilipo?

    Kamwe sinuni bali nanena kwa nuni na kalamu adhimu ya haki ilitotimilivu, iandikayo karatasi nyeupe...peee!!!

    Mwe'macho hambiwi ona,yalojiri yameonwa na walimwengu kote duniani.

    Mithali za dhuluma kwa wazanzibari, imedhihiri batili,sote tulistahili, kukemea jambo hili, yu wapi alo mahiri, kunena pasi hadhari, atekwe awekwe bari, atafutwe na famili.

    Wakatabahu neno hino, lilonenwa kwa nuni, mjuvi wa hino, avinjari katika medani.

    ReplyDelete