Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Itiji(CHADEMA) Ezekiel King ukiwa umetelekezwa baada ya askari polisi kusambaratisha wafuasi wa CHADEMA. |
Jeneza lililobeba mwili likitolewa kutoka chumba cha kuhiofadhia maiti hospitali ya rufaa Mbeya. |
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya mjini John Mwambingija na Mbunge wa MBEYA mjini Joseph Mbilinyi SUGU wakifunika jeneza lenye mwili wa marehemu King. |
Wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na viongozi wao wakitoka nje yaa hospitali ya Rufaa Mbeya na mwili wa marehemu King, kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwao marehemu. |
Mkuu wa Polisi Mbeya mjini(OCD)Richard MCHOMVU akizungumza na Mwenyekiti wa CHADEMA mbeya mjini na kuwataka wapakie mwili wa marehemu kwenye gari badala ya kuandamana barabarani wakiwa na jeneza. |
Mbunge wa Mbeya mjini Sugu, akieleza msmimamo wake wa kutaka wafuasi wa CHADEMA kubeba jeneza na kutembea nalo hadi nyumbani kwa marehemu. |
Mwenyekiti wa CHADEMA mbeya mjini John MWAMBIGIJA akisisitiza kuwa watabeba jeneza na kutembea nalo hadi nyumbani kama walivyopanga. |
OCD Mchomvu akiendelea kuwasiliana na vijana wake wajiandae kwa kazi!! |
Wakati huo huo kundi la wafuasi wa CHADEMA wakiwa na jeneza la mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa SERIKALI ya Mtaa wa Itiji wakianza safari kuelekea nyumbani kwa marehemu |
Safari inaendelea!! |
Safari inaendelea hadi kona ya Kanisa Katoliki mkabala na Kituo cha Polisi Central jijini Mbeya |
Upande wa pili katika kituo cha polisi Central askari polisi wakiwa wamejiandaa wakisubiri amri ya kuanza utekelezaji wa maagizo kutoka kwa mkuu wao |
Msafara wenye jeneza lenye mwili wa marehemu ukiendelea!!! |
Tahamaki!! majira ya saa sita mchana gari la polisi hiloo!!! mabomu ya machozi yakaanza kurindima!! wafuasi wa CHADEMA wakatawanyika!!! |
Jeneza lenye mwili wa marehemu likabwagwa chini polisi wakalizingira na kulichukua na kuliweka kwenye gari lao!!! |
Askari polisi wakiwa wamejipanga kwa lolote!! |
Mara baada ya polisi kuchukua jeneza walilirejesha katika chumba cha maiti hospitali ya Rufaa Mbeya |
Ulinzi uliimarishwa nje ya Hospitali ya Rufaa Mbeya |
Mbunge wa Mbeya mjini Sugu alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa hali inakaa vyema na uitaratibu wa maziko unaendelea kama ulivyopangwa. |
Mazungumzo ya pande mbili yaliendelea kufanyika ili kutyafuta suluhu baina ya polisi na wafuasi wa CHADEMA |
Hatimaye jeshi la polsi walikisadia CHADEMA kutafuta gari kwa ajili ya kuubeba mwili wa marehemu badala ya kutembea nao barabarani hadi nyumbani. |
Wafuasi wa CHADEMA mara hii wakiwa wengi zaidi ya mara ya kwanza wakiusindikiza mwili wa marehemu ndani ya gari wakielekea kanisani. |
Ndugu jamaa na waombolezaji wengine wakiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Itiji wakati wa kuuaga mwili. |
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika makaburi ya NONDE alikozikwa Ezekiel King |
WAFUASI wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
leo asubuhi wamelazimika kuutelekeza barabarani mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti
wa Serikali za Mtaa wa Itiji Ezekiel King(53) baada ya kuvurumishwa kwa mabomu
ya machozi kutoka kwa askari Polisi kikosi cha FFU.
Hali hiyo
iliibuka majira ya saa sita mchana eneo la mnara wa kumbukumbu ya mashujaa
wakati askari hao walipoibuka katikati ya maandamano ya wafuasi hao ambao
walikuwa wameubeba mwili wa marehemu wakielekea nyumbani kwake mtaa wa Itiji na kuwazuia.
Hali hiyo
iliwasabababisha wafuasi wa CHADEMA kuubwaga chini mwili wa marehemu na
kutokomea kusikojulikana na askari hao kuuchukua mwili na kuupakia kwenye gari
lao na kuuridisha chumba cha maiti
hospitali ya Rufaa Mbeya.
Hata hivyo
mara baada ya muda mfupi wafuasi hao walirejea tena na kukutana nje ya chumba
cha kuhifadhia maiti na kusubiri maelekezo kutoka kwa viongozi wao ambao
walikuwa wakifanya mazungumzo na viongozi wa jeshi la polisi.
Mara baada
ya mwili kurejeshwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, viongozi wa chama hicho
pamoja na polisi walikaa na kujadiliana njia bora ambayo ingefaa kumaliza
mgogoro huo uliosababisha kuibuka kwa taharuki hiyo.
Akizungumza
na baadhi ya wafuasi waliohudhuria nje ya chumba cha maiti Mbunge wa jimbo la
Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu aliwaambia wafuasi wake
kuwa wamekubaliana na jeshi la polisi kutembea na kuusindikiza mwili wa
marehemu hadi katika kanisa katoliki.
Awali
wafuasi hao wa CHADEMA walitaka kuuchukua mwili wa marehemu na kutembea nao kwa
miguu hadi nyumbani kwake Itiji lakini Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya Richard
Mchomvu aliwataka wafuasi hao kutotumia njia hiyo na badala yake watafute gari
kwa ajili ya kuusindikiza mwili wa marehemu hadi nyumbani kwake.
Post a Comment