Ads (728x90)

KUNA jambo moja la kimila sijui ni la kidesturi za Kiafrika ama sijui ni ustaarabu wa watu wa ukanda fulani wa sehemu katika nchi yetu linanitia kichefuchefu, hata hapa ninapoanza kupandisha mada hii najihisi kama nimelemewa na mzigo mzito wa maji ‘aka’ mate uliojaa kinywaji kwa minajili ya kutaka kutema ‘aka’ kutapika kwa kujihisi vibaya.

Si kwamba labda binti fulani rafiki yangu kanibebea mimba ndio maana najisikia hivi, kwani kuna itikadi kwamba kama mwanamke uliyekaribu nawe hata kama si Girl Friend wako ‘aka’ mpenzi wako, ana ujauzito anaweza kukuambukiza wewe tabia na mienendo ya hatua zote za ujauzito ikiwa ni pamoja na kupenda kula vitu vyenye ugwadu, udongo n.k.

Kinachonitia kichefuchefu si hilo, bali tabia hii ya baadhi ya watu wa aina fulani katika mila za kiafrika…eti siku ya kumuoza binti yao ili kuthibitisha kama binti huyo alikuwa bado ni BIKRA humualika kungwi ambaye atakuja kushuhudia tendo la ndoa linavyotendeka na yeye kutoa taarifa kwa wahusika kama binti yule alikuwa mzima ama la.

Kwamba siku hiyo mara baada ya kufungwa kwa ndoa mume na mke huandaliwa chumba maalumu mchana kweupe, kukiwa na mashuhuda anuai na kisha hutandikwa kitambaa cheupe katikati ya kitanda kwa minajili ya kuangalia rangi nyekundu (aka) damu ambayo itathibitisha kwamba binti huyo hakupata kuingiliwa kimwili katika maisha yake hadi siku hiyo ya ndoa.

Eti husemwa kuwa mume anapomuingilia mkewe iwapo bado ni BIKRA haruhusiwi kumalizia ndani kwa ndani na kwamba eti yule kungwi ndiye anachukua mamlaka ya kuwa mke kwa muda ule ili kummalizia ashiki zake yule mume(sina ushahidi nalo hilo), lakini kwa yale niliyoyashuhudia kwa mboni zangu mbili zinanifanya nione mila hizi zinatia kichefuchefu na wala hazifai kufuatwa.

Kwamba mara baada ya kujulikana kwamba yule Binti alikuwa ‘MWALI’ basi shangwe vifijo na vigelegele hurindima na kupigwa mbiu kwamba, ndoa imejibu ambapo mama ‘Mzaa Chema’ hupakwa unga mweupe (sijui kwa mila zingine hufanya vipi) na kisha eti mama huyo hupewa tuzo fulani ikiwa ni sehemu ya shukrani za kumtunza bint yake hadi kufikia kuolewa bila kuingiliwa na mwanaume yoyote.

Ukiangalia kwa makini hali ya binti kujitunza na kufikia hatua ya kuolewa kabla ya kuguswa na mwanamume inaleta hamu ya kuisifia hali hiyo na kutoa pongezi hususani katika kipindi hiki kilichozongwa na maradhi ya ugonjwa wa UKIMWI, lakini zile hatua zinazochukuliwa kubani kwaamba binti huyu ni BIKRA zina walakini.

Nina mengi ya kuelezea juu ya hili heebu niwaachie wambuji wa kuchangia mada uga wao(Haya na tuchangie hili na ikiwezekana ipatikane njia mbadala badala ya hiyo iliyopo sasa)

Chemi Che Mponda, Martha Mtangoo, Zainabu Yusuf, Fatma Karama[MM1] , hii ni changamoto kwenu tuelezeni kama njia hii ina manufaa yoyote kwa akina dada ama ni udhalilishaji.

Wakatabahu.


Post a Comment

  1. Aise Mkwinda hivi wewe ulisomea darsa gani? kwenye mti ule wa pale shuleni kwetu au mwembeni?, mbona ulivyokuwa shule haukuwa na maneno ya mistari kama haya!, nahisi sasa tunaweza tukaanzisha bendi kabisa wewe utatunga nyimbo, mimi napiga gitaa, nyembo itabidi apige ngoma, msangi atapiga kinanda......., ila mastedi shooo sijui watakuwa kina nani nahisi nafasi hii itakuwa wazi kwa muda.

    ReplyDelete
  2. DU INATISHA!
    Pongezi kwa makala hii Bw Mkwinda. Nakufahamu kama Mwandishi wa Makala wa Gazeti fulani la kila siku, sijui ni wewe?
    Kuhusu mada yako, ni kwammba
    mila za namna hii zipo, kwani lisemwalo lipo. Cha muhimu ni kupiga marufuku mila hizi kama vile tunavyopinga ukeketaji kwa wanawake. Haiwezekani kungwi akachukua majukumu ya mwanandoa katika mapenzi, si haki na si vema kiafya, ukizingatia hali tete ya UKIMWI iiyopo sasa.
    Endelea kutuelimisha Kaka.
    Karibu 'http://jadili.blogspot.com'

    ReplyDelete