MWANDISHI MAHIRI WA VITABU VYA FASIHI NCHINI NYANGWINE NYAMBARI
AMEELEZA MSIMAMO WAKE JUU YA MUSTAKABALI WA KISIASA NCHINI NA MTAZAMO
WAKE JUU YA MAENDELEO YA NCHI KATIKA NYANJA ZA KIJAMII, KIUCHUMI NA
KISIASA KWA KUSEMA KUWA MIAKA 13 IJAYO ATAJITOSA KUWANIA URAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
NYAMBARI AMBAYE PIA NI
MBUNGE WA JIMBO LA TARIME KUPITIA CCM ALIYECHAGULIWA MWAKA 2010 NA
KUIWEKA RAMANI YA TARIME KATIKA SURA YA CCM BAADA YA MIAKA KUMI KUWA
CHINI YA UPINZANI AMEBAINISHA HAYO KATIKA MAZUNGUMZO MAALUMU NA
WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA.
ALISEMA KUWA TANZANIA KAMA
NCHI NYINGINE ZINAHITAJI MAENDELEO ENDELEVU KATIKA SEKTA ZOTE NA KUWEKA
BAYANA KUWA IWAPO SERIKALI ITAWEKEZA KATIKA ELIMU NA KUJENGA UZALENDO
NA KUJITEGEMEA KWA WANAFUNZI WA NGAZI ZA ELIMU YA AWALI.
''TUKIWEKEZA
KWA WANAFUNZI DARASA LA AWALI KWA KUWAFUNDISHA UJASIRIAMALI HATA
WAKIFIKA ELIMU YA CHUO KIKUU WATAKUWA NA NIDHAMU YA KUJITEGEMEA,
WATAONDOKANA NA UTEGEMEZI WATAISHI MAISHA BORA''ALISEMA NYAMBARI''
ALIFAFANUA
KUWA LUGHA YA UJASIRIMALI INAPASWA KUANZIA NGAZI ZA CHINI NA KUJENGA
MAZINGIRA YA WATU KUJITEGEMEA NA KUJITUMA NA HIVYO KUONDOKANA NA
KULALAMIKA MARA KWA MARA NA MWISHO WA SIKU KUUNDA TAIFA LA WALALAMISHI.
ALISEMA
MFUMO WA ELIMU ULIOPO UNAJENGA MATABAKA YA WALIONACHO NA WASIO NACHO
AMBAPO WALE WENYE NACHO WATOTO WAO HUWAAPELEKA KATIKA SHULE ZENYE MRENGO
WA KITAALUMA WA NCHI ZA NJE ILHALI WALE WASIO NA UWEZO WAZAZI WAO
WAKIWAPELEKA KATIKA SHULE ZA ST. KAYUMBA.
ALIBAINISHA
KUONDOA HALI HIYO MITAALA YA ELIMU IBORESHWE HUKU KISWAHILI KIKIPEWA
KIPAUMBELE KUWA NI LUGHA RASMI YA KUFUNDISHIA NA KIINGEREZA KIBAKI KUWA
NI LUGHA YA MAWASILIANO NA BIASHARA.
''NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA ZINATUMIA LUGHA ZAO NA MAENDELEO YAO YAKO JUU''ALISEMA.
|
Riwaya ya msomi aliyebinafsishwa nimepata kuisoma si chini ya mara tano, riwaya hii ni mojawapo kati ya riwaya zinazungumzia matatizo ya uongozi barani Afrika hasa Tanzania!.
ReplyDeleteRiwaya hii inasawili vizuri aliyotenda mwandishi wake kipndi akiwa mbunge jimboni mwake!!!!!
Hakika fasihi ni tunu kubwa kwa mwanadamu na ikitumiwa vizuri ni silaha tosha kimapinduzi lakini ikitumiwa vibaya itapumbaza jamani, kuipotosha na kukosa uaminifu katika jamii yake!
Mungu ibariki fasihi ya kiswahili!