Misukosuko ya Maisha humfanya mtu kuhisi kuna maadui wanamzunguka!!!!, bali ndiyo aina ya maisha ili dunia iende, mara zote binadamu hudhani kaumbwa ili astarehe tu hapa duniani bila kupata misukosuko ya maisha, bali misukosuko humpa mtu weledi wa kupambana na matukio ambayo kwayo hudhani kuwa ni matatizo isipokuwa huja ili kumpima aina ya uwezo wake wa kuhimili matatizo yanayojiri mbele yake.
Ni wajibu wa binadamu kukabiliana na misukosuko anayoipata, na hiyo ndiyo desturi kwa kiumbe yoyote aliyepo chini ya jua, aghalabu misukosuko humkumba binadamu,kwani ndiye mara zote anawajibika kwa namna moja ama nyingine kujiandalia maisha yake ya kila siku, maisha yajayo na kutengeneza familia yake.
Ingawa wapo watu wanaodhani kuwa misukosuko ni matatizo.Bali wanachopaswa kukijua ni kwamba misukosuko ni sehemu ya maisha na ni wazi kuwa hakuna aliyeumbwa kuwepo katika misuko suko daima, misuko suko huja ili mtu ajifunze aina ya maisha aliyonayo ikiwezekana aanze mchakato wa kukabiliana na aina hiyo ya misukosuko na hata kuanzisha mtindo mwingine wa maisha.
Wapo watu wanadhani kuwa wameumbwa kuwasababishia misukosuko wengine wakidhani kuwa misukosuko imeumbiwa watu fulani na jamii fulani, La hasha kila aliyetokana na ADAMU ni wajibu kwake kukumbwa na misukosuko kwani huo ni urithi ambao umeasisiwa na Baba yetu Adam na mama yetu Hawa, haiwezekani kuikwepa misukosuko asilani!! abadani!!
Tumeshuhudia wengi waliokumbwa na misukosuko awali na baadaye kuwa katika maisha bora yenye furaha, kadhalika tumeshuhudia wengi waliokuwa katika maisha bora na fanaka wakiwa katika misukosuko, huu ni mfano mzuri kwa mnasaba wa jinsi dunia ilivyoumbwa, kwani imeumbwa DUARA.Kilea ambacho utakosa kukipata leo kitapita katika mzunguko na hatimaye utakuja kukipata kwa wakati mwingine, lakini pia ukiweka nia na jitihada mbele.
Nini cha kufanya ili misukosuko isiwe sehemu ya matatizo kwa binadamu!!?....jambo la muhimu hapa ni kukubali kupata misuko suko kwani ni sehemu ya maisha, wengi waliokumbana misukosuko tumewaona wako katika faraja....kama usemavyo msemo kuwa BAADA YA DHIKI FARAJA.
Wakatabahu!!!!!!!
Yote umesema kaka.
ReplyDelete