Hii ndio Telemka Tukaze
Wakumbuka aina hii ya Kitanda, nadhani vijana wengi wa sasa hawavijui aina hii ya vitanda vya ukambaa, hii ilikuwa ni kazi za mikono za mababu zetu enzi hizo na hata wengine walidiriki kulalia ngozi, ustarabu wa kigeni ndio umetupeleka hadi hapa tulipo kudharau enzi zetu.Aghalabu wa enzi hizo hawakuwa wakiumwa migongo sana na kulala kwao ilikuwa ni sehemu ya mazoezi, wakiamka asubuhi walikuwa hawana haja ya kufanya sana mazoezi, kwani kulala tu pekee ilitosha kuwa ni sehemu ya mazoezi, sasa hivi vijana wanajikuta wapo katika utandawazi eti kwa kulala katika vitanda vya futi sita kwa sita vyenye sponji na vono mumo kwa mumo. Hebu tujaribu kurejea enzi zile. Nani anaweza kujaribu kulalia aina hii ya kitanda kwa wakati huu?
Post a Comment
Post a Comment