Wanafamilia hawa wa kijiji cha Isuto Mbeya vijijini wamelazimika kutembea kilomita 30 wakiwa na mtoto wao mgonjwa kwa ajili ya kumpeleka katika zahanati iliyopo kijijini hapo. Kwa mujibu wa wanafamilia hao wamesema kuwa wanakoishi ni mbali sana hakuna aina yoyote ya usafiri, mtoto wao alianza kuumwa usiku na wao kuamua kumbeba mgongoni na kutembea kuanzia saa saba usiku hadi saa saba mchana ambapo wamefika katika kituo cha afya Isuto ambacho pia wamekosa matibabu kwa kukosekana kwa dawa.
Ina maana mbunge wao Marehemu Nyaulawa hakuweza kufanya chochote katika kutatua kero hiyo ya wana nchini ,ama hii ni mbeya vijijini ya jimbo gani kaka ,kweli inasikitisha sana lakini ni moja ya changamoto kubwa kwa wannachi kuweka mikakati ya kuchagua vipaumbele vyao ili serikali kupitia mfuko wa TASAF waweze kusaidiwa lakini kama wameweka viongozi mbumbumbu wameula picha nzuri
ReplyDeleteNdugu yangu Marehemu Nyaulawa hakukaa muda mrefu katika jimbo hilo na alikuwa amekwisha anza mikakati maalumu ya kuwahakikishia kuwa wanaishi maisha bora., alianza mchakato wa kuanza kujenga kwianda cha pembejeo za kilimo, akiamini kuwa tatizo kubwa linalosababisha ukata kwa wananchi wa jimbo lake ni kukosa pembejeo za kilimo na hiyo ilikuwa ni hatua ya awali kuelekea katika kuwatimizia wapiga kura zake baadhi ya kero ambazo zipo katika maeneo yao.
ReplyDelete