Ads (728x90)

Hebu na tutafakari upya inawezekana mwaka 2010 bila katiba mpya na tume ya uchaguzi iliyo chini ya mfumo wa chama kimoja? mmeamua kuingia tena katika kinyang'anyiro, mnawaahidi nini wapiga kura iwapo kitakachotokea ni sawa na kile kilichojiri miaka iliyopita?
Napata kigugumizi kwamba uchaguzi wa mara hii kwamba unaweza kuwa ni tofauti na ule wa miaka iliyopita lakini kwa kuwa ninyi waheshimiwa mmeamua kujitosa tunatarajia mnaweza kushinikiza angalau uchaguzi huu uwe huru na haki, hatudhani kama kutakuwa na kiswahili cha kupinga matokeo.
Mmeddhamiria kunena kwa kinywa chenu kwamba mmeamua kujitosa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, nadhani mnakumbuka kuwa tume iliyopo inakidhi mfumo wa chama kimoja cha kisiasa, haina ridhaa ya mfumo wa vyama vingi, mnataka kutuambia tujifunze nini katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?yetu macho kuona na masikio kuona na miguu kukimbia zahama na mabomu ya wagammbo waliofunzwa rasmi kupambana wakati wa uchaguzi mkuu kudhibiti upinzani.

Post a Comment

  1. tumechoka kuwaona nyie tu kila siku tunaomba sura zingine zijitokeze zinaweza kuja na mawazo tofauti na mlio nayo nyinyi na tukaafiki na kupata msukumo wa kubadili mawazo yetu na kuchagua cuf sasa walewalena mawazo ni yaleyale yaliyowaangusha miaka ile leteni sura mpya na sera nina uhakika zitakuwa mpya na mambo yatakuwa mapya nasi tutbadili mwelekeo.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa sura zikiwa za zamani na mambo huwa ni ya zamani, ili kuleta mabadiliko zije sura mpya ili ziwe na mambo mapya.

    ReplyDelete