Ads (728x90)

MKUU WA MKOA WA MBEYA JOHN MWAKIPESILE USIKU HUU NUSURA AONJESHWE NYAMA YA PANYA MAARUFU KWA JINA LA SAMAKI NCHANGA KATIKA USIKU WA VYAKULA VYA ASILI AMBAVYO VILIANDALIWA NA MAKABILA MBALIMBALI YA MKOA WA MBEYA,MKUU HUYO AMBAYE PIA ALIAMBATANA NA WAKUU WENZIE WA MIKOA YA RUKWA DANIEL OLEY NJOOLAY(RUKWA) DKT.CHRISTINE ISHENGOMA(RUVUMA)WALIKUWA KATIKA SEHEMU YA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA NANE NANE
SHEREHE HIZO HUFANYIKA KIKANDA KILA MWAKA NA KUHUSISHA MIKOA YA IRINGA,RUKWA,RUVUMA NA MBEYA,USIKU HUU ULIKUWA RASMI IKIWA NI MGAWANYIKO WA SIKU NNE KWA KILA MKOA KUONESHA UMAHIRI WA MAMBO YA KIASILI IKIWA NI PAMOJA NA KUCHEZA NGOMA,MAPISHI YA VYAKULA VINAVYOPATIKANA KATIKA MIKOA HUSIKA NA MAMBO MENGINE.
MIKOA HII NDIYO ILIYOBEBA DHAMANA YA CHAKULA NCHINI AMBAYO KUTOKANA NA UMAARUFU WAKE WA UZALISHAJI WA CHAKULA ILIFIKIA KUITWA NI MIKOA YA THE BIG FOUR,KWA SASA MIKOA MAARUFU YA UZALISHAJI WA CHAKULA NI SITA IKIWEMO MIKOA YA MOROGORO NA KIGOMA.

Post a Comment

Post a Comment