Ads (728x90)

(KUMRADHI) TUMELAZIMIKA KUACHA BAADHI YA PICHA ZA AJALI HII KUTOKANA NA HALI HALISI YA KUTHAMINI UTU WA BINADAMU KWANI BAADHI YA PICHA HIZO ZINATISHA SANA)

Matukio ya ajali katika mkoa wa Mbeya yameendeela kutishia uhai wa wasafiri abapo kwa juma moja takribani watu 26 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali zilizotokea katika maeneo ya Mbalizi, Msangamwelu na Mbozi katika kitongoji cha Chimbuya.
Ajali iliyotokea Msangamwelu wilayani Chunya iligharimu maisha ya watu 14 ambapo ajali iliyotokea Mbalizi iligharimu maisha ya watu watatu ilhali ajali ya leo asubuhi katika kitongoji cha Chimbuya imegharimu maisha ya watu 9 ambao walikuwa katika safari kati ya Tundfuma na Mbeya.
Ajali hiyo imehusisha Kipanya Toyota Hiace yenye namba za usajili T 219 ASW iliyokuwa ikisafiri kutokea Tunduma kuelekea Mbeya na Landcruiser Prado yenye namba za usajili T 155 iliyokuwa ikitokea Mbeya kuelekeaa Tunduma kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 9 na kujeruhi wengine 12.

















(PICHA KWA HISANI YA INDABA AFRICA-MBOZI)

Post a Comment

Post a Comment