Ads (728x90)

NI siku tatu za huzuni na maombolezo nchini baada ya meli ya Mv SPICE Islanders kuzama katika bahariya Hindi maeneo ya Nungwi mudas mfupi baada ya kung'oa nanga katika Bandari ya Malindi mjini Unguja.
VIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR, RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS MAALIM SEIF SHARIF HAMAD NA MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN WAKISHUHUDIA UOPOAJI WA MIILI YA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA MELI
VIONGOZI WA SMZ RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN,MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD NA MKE WA RAIS WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA TUKIO LA KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDER
Inakadiriwa watu zaidi ya elfu moja walikuwemo katika meli hiyo ambayo pia ilisheheni mizigo lukuki kama vile magodoro, unga na mchele.
MIILI YA WATU WALIOKUFA MAJI KATIKA MELI YA SPICE
Wengi waliofariki katika ajali hii wanaelezwa kuwa ni akina mama na watoto ingawa hadi sasa idadi kamili ya waliokufa katika ajali hiyo hawajajulikana bali maiti zipatazo 200 zimeopolewa katika maji huku abiria zaidi ya 600 wameokolewa na wanaendelea kupatiwa matibabu kwa gharama za serikali.
BAADHI YA WATOTO WALIOKOLEWA KATIKA MELI ILIYOZAMA VISIWANI ZANZIBAR
Aidha tukio hilo la kuzama kwa meli ni muendelezo wa matukio ya aina hii hususan katika vyombo vya usafiri nchini iwe nchi kavu na majini, ambapo kwa kipindi kisichozidi miaka miwili meli nyingine ya mizigo Mv Faith nayo ilizama visiwani humo na kusababisha vifo vya watu sita, ambapo pia hadi leo nchi yetu inakumbuka ajali ya meli ya MV BUKOBA iliyozama katika Ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu wanaokadiria kufikia 800 ambapo sababu za kuzama kwa meli hiyo zinashabihiana kabisa na tukio tulilonalo hivi sasa.
WAOKOAJI WAKIWA NA MIILI YA WATU WALIOKUFA AJALINI
Kama ilivyo kwa desturi ya binadamu linapotokea tukio la simanzi kama hili kila mmoja atazungumza lake kulingana na hisia zake ili mradi afikishe ujumbe unaoshabihiana na tukio lilivyo.
Ingawa ni kweli kutokea kwa tukio hili kunaweza kuwa kunatokana na matatizo ya kiufundi ama sababu nyinginezo, lakini ukweli utabaki pale pale kwamba ndugu zetu wamehiliki baharini na wameangamia hawapo tena duniani.

Yapo mengi yatakayozungumzwa juu ya tukio hili! lakini jambo la muhimu hapa ni kutafakari kwa kina sababu hasa za matukio ya aina hii ambayo kwa utashi wa kawaida unaohanikizwa na jazba zetu za kibinadamu tutasema kuwa kuna watu wamesababisha kutokea kwa ajali hiyo.

Siamini kama kweli kama kuna mmoja wetu anaweza kuamua kwa makusudi kusababisha ajali ya aina hiyo ambayo imegharimu maisha na nguvu kazi za Taifa letu. Ukweli ni kuwa bahati mbaya imetokea.tutafakari kwa hekima juu ya ajali hii ili tupate sababu za kujikinga kutotokea.

Post a Comment

Post a Comment