TAHARUKI JENGO TRA MBEYA LANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO
TRA WAFANYAKAZI wapatao 70 na wateja wa Mamlaka ya Mapato TRA mkoani Mbeya leo mchana wamekumbwa na taharuki baada ya jengo la mamlaka hiyo kuhofia kutetetea kwa moto.Taharuki hiyo imetokea baada ya kusikika mlio wa king'ora kilichomo ndani ya jengo hilo na kusababisha wafanyakazi na wateja kutimua mbio.
Hatua hiyo ilisababisha uongozi wa Mamlaka ya Mapato kuita Kikosi cha Zimamoto ambapo pia wafanyakazi hao kila mmoja aliacha kazi zake na kuteremkaa chini.
Wakizungumza eneo la tukio wafanyakazi wa Mamlaka hiyo walisema kuwa waliwahi kutahadharishwa kuwa iwapo king'ora ambacho kimeweka kuashiria hatari kikilia wanatakiwa kutoka ndani ya jengo hilo ili kuepuka hatari ya moto inayoweza kutokea.
Meneja Mkuu msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mbeya Bw. Sidney Mkamba alisema kuwa king'ora hicho kimeanza kulia saa saba na robo mchana ambapo baada ya muda mfupi kilizimwa, na kwamba mara baada ya kusikika kwa mlio huo waliwasiliana na watu wa zima moto na TANESCO ili kuangalia uwezekano wa kuzuia hatari hiyo.
Post a Comment
Post a Comment