Watoto 32 wamezaliwa katika mkesha wa kuamkia sikukuu ya krismas mkoani Mbeya,Wakristo duniani kote wanasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Watoto hao wamezaliwa katika hospitali tofauti zilizopo ndani ya jiji la Mbeya ambazo ni Hospitali Teule ya Ifisi, Meta, Ruanda na Kiwanja Mpaka. Akizungumza leo mchana Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Rufaa ya Wazazi ya Bw. Frank Sanga alisema kuwa katika mkesha huo jumla ya watoto 17 walizaliwa 12 wakiwa ni wakiume na 5 wa bkike. Alisema watoto hao walizaliwa kati ya saa 8 usiku na asubuhi ya jana ambapo kati yao wawili ni mapacha na kuwa hali zao zinaendelea vizuri. Aliongeza kuwa watoto hao watano walizaliwa kwa njia ya upasuaji na 12 walizaliwa kwa njia za kawaida. Katika Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya iliyopo Ifisi Muuguzi wa zamu hospitalini hapo Bw.Alexander Linus alisema katika mkesha huo watoto 10 walizaliwa wakiwemo wa kike watano na watoto wa kiume watano na kuwa hakuna mzazi wala mtoto ambaye alikuwa na matatizo ya kiafya. Kwa mujibu wa Muuguzi wa zamu wa kituo cha Afya cha Kiwanja Mpaka iliyopo Sokomatola jijini hapo Bi.Tungulilege Ngodo alisema kuwa mtoto mmoja wa kike pekee ndiye aliyezaliwa. Nacho Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Ruanda kilichopo Mwanjelwa Bi Asha Gasper alisema kuwa jumla ya watoto wanne ndio waliozaliwa katika kituo hicho. Katika hospitali ya Mkoa akina mama wajawazito watatu walifikishwa hapo ambapo kutokana na kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida walikibizwa katika hopitali ya wazazi Meta kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. STORI KWA HISANI YA DOTTO MWAIBALE |
Post a Comment
Post a Comment