|  NA, RASHID MKWINDA,MBEYA. WASICHANA wameongoza katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa ajili ya  kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na  mtihani uliofanyika Septemba mwaka huu mkoani Mbeya, huku mwanafunzi wa shule ya msingi  ya Airport ya jijini Mbeya Vaileth Sanga akishikilia usukukani kwa kupata alama 225. Mwanafunzi mwingine  aliyepata alama 225 ni John Mwaipopo kutoka katika shule ya binafsi ya UWATA  ambapo idadi ya wasichana waliochaguliwa kujiunga na sekondari ni 22,104. Akitangaza matokeo hayo Ofisa elimu wa mkoa wa Mbeya Bw. Juma Kaponda alisema kuwa idadi hiyo ya wasichana iko juu dhidi ya wavulana ambao ni 21,136 kati ya watahiniwa 78,667 ambayo ni sawa na wasichana 41,226 na wavulana 37,240.  Alisema kuwa idadi hiyo ya ufaulu ni sawa na asilimia 55 ambapo jumla ya waliochaguliwa kujiunga na sekondari za bweni ni  262 ambao ni wavulana 176 na wasichana  86 ilhali waliochaguliwa katika shule za kutwa ni 32,371 ambao kati yao ni wasichani 16,389 na wavulana ni 15,982. | 
Post a Comment