UZINDUZI wa kampeni za uchaguzi CCM kata ya Kiwira wilayani
Rungwe umeingia na dosari baada ya mmoja wa mashabiki wa chama hicho Frank
Mwasanu(19)aliyekuwa akiendesha pikipiki kujiingiza katika Hiace yenye namba za
usajili T 527 AEP na kufa papo hapo.
Tukio hilo
limetokea majira ya saa 8:00 mchana wakati wa shamra shamra za kampeni za
mgombea wa CCM Peter Nkanje ambapo makundi ya watu walikuokuwa ndani ya
pikipiki walikuwa wakivinjari huku na huko katika harakati za kupamba uzinduzi
wa kampeni hizo.
Mashuhuda wa tukio hilo
walisema kuwa marehemu alikuwa na kundi la wafuasi wa chama chake ambao
walikuwa wakikimbiza pikipiki kwa mwendo wa kasi na baadaye kijana huyo
alijiingiza chini ya mvungu wa Hiace ambayo ilikuwa ikielekea Tukuyu.......
Post a Comment
Post a Comment