Ads (728x90)

WATU 10 wamekufa hapo hapo na wengine 19 wamejeruhiwa baada ya basi aina ya Coaster lenye namba za usajili T 886 BDZ linalofanya safari zake kati ya Mbeya Tukuyu kugongwa na Lori lenye namba za usajili T 658 ASJ lenye Trela namba T 150 ASN maeneo ya Ntangano Jijini Mbeya.

Ajali hiyo imetokea majira ya mchana wakati basi hilo likiwa safarini kuelekea Tukuyu wilayani  ambapo  Lori lenye Trela lilikuwa likielekea Jijini Mbeya kutokea Tukuyu wilayani Rungwe.

Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Jiji Mbeya na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.







Post a Comment

Post a Comment