Mara nyingi baadhi ya watu hususani akina mama wamekuwa na desturi ya kutembelea kwa waganga wa kienyeji 'SANGOMA' kwa ajili ya kutafuta namna ya kutatua matatizo yao yanayowakabili ikiwemo masuala ya kinyumba, kibiashara na mengineyo mfano wa haya.
Wengi wao hutembelea kwa akina Sangoma kwa ajili ya kusafisha nyota zao wakiamini kuwa ndio wanaoweza kutatua matatizo yao kama vile, kuyumba kwa ndoa, biashara na mikosi mbalimbali, hata hivyo asilimia kubwa ya waganga hao wakienyeji wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuwadanganya wanawake wanaofika kwao na kufanya nao vitendo vya ngono.
Mmoja wa wahanga wa matukio ya waganga wa kienyeji amesimulia mtandao huu kuwa, waganga hao huwaeleza masharti magumu wanawake wanaofika kwa ajili kusafisha nyota ikiwemo kufanya ngono.
Mganga alinieleza kuwa dawa ya kusafisha nyota kuondoa mkosi katika ndoa na kupata mtoto lazima zitumike tupu mbili za kike na kiume na kwamba inalazimika uwepo muingiliano baina ya tupu hizo huku tupu moja ikiwa imepakwa dawa, ndipo dawa hiyo huweza kufanya kazi vizuri.
'' Alisema inabidi aingize tupu yake katika tupu yangu ikiwa imepakwa dawa, tatizo langu litamalizika, nilikuwa na tatizo, mikosi iliniandama, ndoa yangu ilikuwa hatarini,biashara zangu zilikwama, lakini hata baada ya kuingiliwa na sangoma bado hali haijawa nzuri, zaidi najihisi kama na ujauzito wa sangoma kwani aliniingilia bila kondomu,''alisema, mwanamama huyo aliyejazia jazia chini ya kiuno.
BLOGU HII INAWATAHADHARISHA AKINA MAMA WOTE NCHINI KUTOPENDELEA KWENDA KWA WAGANGA KWA AJILI YA KUTATUA MATATIZO YAO PICHA JUU ILIYOTOKANA NA MSAADA WA MTANDAO WA JAMIIFORUMS KUPITIA CHANZO CHA http://4.bp.blogspot.com INAONESHA HALI HALISI WANAYOKUMBANA NAYO AKINA MAMA WENGI WANAOTEMBELEA KWA WAGANGA WA KIENYEJI.
Post a Comment
Post a Comment