Ujumbe mzito wa Bill & Melinda Gates Foundation kutoka
Marekani ukiongozwa na Senior Programme Officer (Market Access) Richard
Rodgers ulitua leo kwa ndege ya kukodi kwenye ofisi za Kapunga Rice,
Chimala na kufanya mazungumzo na George Mtenda wa Mtenda Kyela Rice
Supply Company ya Mbeya.
Rodgers
alifuatana na Karen Harkono na Niraj Varia na kwa upande wa Mtenda
Kyela Rice wawakilishi walikuwa Emile Malinza, Josiah Nyato na Jesko
Linga.
Gates Foundation
waliridhika na maelezo yakinifu kutoka Mtenda Kyela Rice na wameahidi
kusaidia katika nyanja za mafunzo kwa wakulima na upatikanaji wa
pembejeo za
kilimo.
Mazungumzo kati
ya pande hizo mbili yanaendelea na mwelekeo
utapatikana baada ya miezi minne kuanzia sasa kwani Rodgers ameahidi
kuwasiliana na ofisi zao za Marekani na kuwapa mrejesho wa ziara yake.
Post a Comment
Post a Comment