MTANDAO UNAODAIWA KUWA CHINI YA WAZIRI MSTAAFU EDWARD LOWASA UMEVUNJWA MKOANI MBEAY BAADA YA MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI GODFREY ZAMBI KUSHINDA UENYEKITI WA MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO.
ZAMBI AMBAYE ALIKUWA KATIKA MCHUANO MKALI NA ALLAN MWAIGAGA MWAJI ALISHINDA KWA KURA 888 HUKU MWAIGAGA AKIPATA KURA 416 AMBAPO REGNAD MSOMBA AMBAYE ALIKUWA MWENYEKITI VIJANA UVCCM MKOA WA MBEYA ALIAMBULIA KURA 168 ILHALI PRINCE MWAIHOJO AMBAYE MWAKA 2010 ALIGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CUF ALIAMBULIA KURA 16.
TAARIFA ZINAELEZA KUWA KATI YA WAGOMBEA HAO MGOMBEA MMOJA WAPOANADAIWA KUFADHILIWA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU KWA KILE KILICHOELEZWA KUWA NI MAANDALIZI YA KUWANIA URAIS WA MWAKA 2015.
AIDHA KUSHINDWA KWA MWAIGAGA AMBAYE AMEKUWA AKIKIFADHILI CHAMA HICHO KWA MAMBO MBALIMBALI KUNAELEZWA KUWA NI KUTOKANA NA YEYE PAMOJA NA ALIYEWAHI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA KATIKA KURA ZA MAONI TOMAS MWANG'ONDA KUSAIDIA USHINDI WA JOSEPH MBILINYI KWA TIKETI YA CHADEMA MKOANI MBEYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment