BAADHI YA WANANCHI WAKISHUHUDIA MAJERUHI WA AJALI |
LORI LILILOSABABISHA AJALI NA KUUA WATU WATANO NA KUJERUHI WENGINE 130 |
( |
(STORI NA RASHID MKWINDA PICHA KWA HISANI YA KAMANGA)
WATU watano
wamekufa na wengine 130 kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyohusisha lori la
mwekezaji kampuni ya Kapunga lenye namba za usajili T 398 BSE aina ya TIPER
SCANIA kupinduka katika kijiji cha Matebete wilayani Mbarali leo asubuhi.
Lori hilo
lilikuwa limebeba vibarua ambao walikuwa wakienda kupalilia katika shamba la
Mpunga na mwekezaji huyo ililopo katika kijiji Mapogoro ambapo miongoni mwao
walikuwepo baadhi ya wanafunzi walioacha shule na kwenda kufanya kibarua katika
shamba hilo.
Mashuhuda
wa ajali hiyo waliofika eneo la tukio walidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
dereva wa Lori kufukuzana na mwendesha pikipiki aliyekuwa amelipita gari hilo
hivyo alianza kushindana nalo ili alipite.
Aidha
waliokufa katika hiyo wamedaiwa kuwa ni watu watano wawili wakiwemo mwanamke na
mwanaume waliofia Hospitali ambapo kamanda Athumani alipata taarifa za vifo vya
watu watatu waliokufa papo hapo katika
ajali.
Kwa mujibu
wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amesema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:15
asubuhi ambapo dereva wa Lori hilo aliyefahamika
kwa jina la Baraka Molel(29) alikuwa
katika mwendo kasi.
Amewataja
watu waliokufa katika ajali kuwa ni pamoja na Samwel Mapugilo(30) mkazi wa
Ilembula,Ben Mfupa(27) mkazi wa Mapogoro na Edgar Mwakipesile(35)mkazi wa Nonde
Jijini Mbeya.
Kamanda
Athumani amesema kuwa wakati gari hilo linakwenda vibarua waliokuwemo ndani ya
gari hilo walikuwa wakishangilia hivyo kusababisha dereva huyo kuongeza mwendo
na kusababisha ajali hiyo.
Kamanda
Athumani amesema kuwa watu 130 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambapo baadhi yao
wamelazwa katika hospitali ya Misheni Chimala wakiwemo wanaume 89 na wanawake 41 ambapo kati yao wanaume 49 na
wanawake 25 na majeruhi wengine 56 wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein Kifu
walikuwa ni miongoni mw amashuhuda wa ajali hiyo ambao walifika katika
hospitali ya Misheni Chimala na kushuhudia umati wa watu waliokuja kuwajulia
hali ndugu zao.
Akizungumza
hospitalini hapo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw.Kandoro aliwapa pole majeruhi na kuwataka
wananchi kujitokeza kuchangia damu katika ajali hiyo ambapo alisema serikali
imepeleka dawa na madaktari kusaidia kuwatibu majeruhi.
Pia amemtaka
mwekezaji kusaidia chakula kwa majeruhi waliolazwa katika hopitali hiyo
kutokana na kwamba asilimia kubwa ya majeruhi waliolazwa hapo ni wakazi wa nje
ya eneo hilo.
Aidha ilidaiwa
kuwa Lori hilo lilikuwa na abiria zaidi ya 200 ambao walikuwa na kawaida ya
kupelekwa katika mashamba ya mwekezaji wa Kapunga na kurejeshwa jioni.
|
Post a Comment